Ushindi waipa mzuka Zanzibar Heroes

BAO pekee lililowekwa kimiani na nahodha, Feisal Salum ‘Fei Toto’ limeiwezesha timu ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes kuanza vyema michuano ya Kombe la Mapinduzi 2025 kwa kuichapa Kilimanjaro Stars ya Tanzania Bara kwenye pambano la ufunguzi wa michuano hiyo lililopigwa Uwanja wa Gombani, kisiwani hapa.

Pambano hilo la wanandugu, lilipigwa usiku wa jana na Fei Toto kufunga bao hilo dakika ya 52 baada ya Daud Semfuko kupokwa mpira wa pasi kutoka kwa beki Lameck Lawi na wachezaji wa Zanzibar kufanya chapu kupasiana na Fei kuumaliza wavuni kuipa timu hiyo ushindi huo uliopokewa kwa furaha na wenyeji.

Katika mchezo huo ambao haukuwa na kuvutia kutokana na timu zote kukamiana zaidi kabla ya mambo kubadilika kipindi cha pili na wenyeji kupata bao hilo lililowapa pointi tatu muhimu wakati michuano hiyo inayoshirikisha timu nne ikiendelea leo kwa pambano la Burkina Fado dhidi ya Harambee Stars ya Kenya.

Mara baada ya pambano hilo, kocha wa Zanzibar Heroes, Ali Bakar Mngazija alisema ushindi huo unatokana na maandalizi mazuri walioyoyafanya.

Mngazija alisema haukuwa rahisi kuifunga Kili Stars kutokana na ushindani uliokuwepo lakini anashukuru  kwa vijana wa Zanzibar Heroes kufuata maelekezo jambo lililochangia ushindi huo muhimu ambao ni mwanzo mzuri kwao katika michuano ya Mapinduzi inayoshirikisha timu za taifa badala ya klabu kama ilivyozoeleka.

ZN 01

Kocha huyo alisema ushindi huo hauwafanyi wabweteke kwani bado kuna michezo mingine miwili migumu dhidi ya Burkina Faso na Kenya, hivyo wanaenda kusahihisha makosa yaliyojitokeza mbele ya Kili Stars kisha kujiweka sawa kabla ya mechi hizo zijazo. Zanzibar itavaana na Burkina Faso keshokutwa, Januari 6 kwenye Uwanja wa Gombani kunakofanyikia michuano hiyo itakayofikia tamati Januari 13.

“Tunashukuru kwa kuanza michuano kwa ushindi huu, niwapongeze wachezaji wangu wamecheza vizuri kwa kufuata maelekezo tuliyowapa naamini kwa mwendo huu utashinda na michezo mengine licha ya ushindani uliopo,” alisema Mngazija, huku kocha wa Kilimanjaro, Ahmad Ali alijitetea wamefungwa kwa bahjati mbaya kwani pambano lilikuwa fifte fifte na kuwapongeza Zanzibar kwa kutumia nafasi moja waliyoipata kuwapa ushindi.

Ahmad amesema tayari dosari zilizojitokeza atakwenda kuyafanyia kazi na kujipanga na mchezo mwengine aweze kupata matokeo mazuri na kuwataka mashabiki na wapenzi wa timu hiyo kutovunjika moyo watashinda mchezo ujao.

Alisema watawasoma Harambee Kenya watakaovaana nao Januari 7 katika mechi ya leo Jumamosi dhidi ya Burkina Faso ili kujua namna ya kuwakabili.

ZN 02

“Tukubali tumefungwa mchezo haukuwa mgumu kiasi hicho wala haukuwa rahisi ni matokeo ya kimchezo lakini tutayafanyia kazi mupungu yaliyojitokeza na tutawasoma wapinzani wetu Kenya tutakao kutananao katika mchezo ujao hata tukicheza nao itakuwa tumesha wasoma,” alisema.

Related Posts