Na Issa Mwadangala
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Augustino Ignace Senga ametoa Zawadi kwa askari waliofanya vizuri katika kazi za Polisi baada ya kukagua mazoezi yaliyoandaliwa na Kikosi cha kutuliza Ghasia Mkoa wa Songwe.
Zawadi hizo ni pamoja na pesa taslimu zilizotolewa Januari 04, 2025 na kueleza kuwa kipekee ameanzisha utaratibu wa kutoa zawadi kwa askari wanaofanya vizuri katika mambo mbalimbali katika kazi za Polisi kwa lengo la kujenga uwezo nakutatua changamoto za jamii ili wananchi waendelee kuwa na imani na Jeshi la Polisi” amesema Kamanda Senga.
Amesema zawadi hizo zinalenga kutambua na kuthamini jitihada za askari wanaofanya vizuri na ameahidi zoezi hilo kuwa endelevu Mkoani humo.
Sambamba na hilo, Kamanda Senga amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IJP) Camillus Mongoso Wambura kwa kuendelea kutatua changamoto za Jeshi la Polisi hasa katika suala la rasilimali watu na vifaa.