CCM IRINGA WATOA SHUKRANI KWA WANANCHI

NA DENIS MLOWE, IRINGA

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa, Daudi Yassin, amesema kuwa ushindi mkubwa walioupata katika uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji, na vitongoji imetokana na utekelezaji wa ilani ya chama hicho chini ya Rais Samia Suluhu Hassan na kuwashukuru wananchi kwa kuwapigia kura.

Yasin alisema hayo wakati akizungumza na wanahabari mkoani hapa katika kikao kilichokuwa na malengo ya kuwashukuru wananchi na wanahabari kwa kuwezesha ushindi mkubwa waliopata katika chaguzi ya serikali za mitaaa.

Alisema kuwa ushindi huo umethibitisha mafanikio ya utekelezaji wa ilani ya chama hicho, ambayo imeleta maendeleo kwa wananchi kuanzia ngazi ya chini na kufanya wananchi kuendelea kukiamini chama cha Mapinduzi.

Yassin aliongeza kuwa ushindi huo ulitokana na mchakato uliyoendeshwa kwa umakini na kuzingatia maslahi ya wananchi kuanzia ngazi zote za jamii mtaa, kijiji hadi ngazi ya taifa.

Alisema kuwa chama hicho kilijipanga vizuri, na hakikuwa na mpango wa kushinda kwa bahati, kama baadhi ya watu wanavyodhani, bali ilikuwa ni matokeo ya utekelezaji wa sera bora za maendeleo na ushirikiano wa karibu na wananchi katika utekelezaji wa ilani ya ccm.

Alisema uthibitisho wa kujipanga katika uchaguzi huo ni ushindi wa asilimia 99.99…, jambo ambalo limeleta imani kubwa kwa wapiga kura.

Aidha alisema siri kubwa nyingine ya ushindi ni kuchagua wagombea wanaokubalika ndani ya jamii wanayoishi.

Alitumia nafasi hiyo kutoa shukrani kwa wanahabari na wananchi wote wa Iringa kwa ushirikiano wao mkubwa ambao ulisaidia chama cha mapinduzi kuibuka na ushindi huo wa kishindo.

 

Related Posts