SACP SENGA – FANYENI KAZI KWA KUZINGATIA SHERIA

Na Issa Mwdangala


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Augustino Ignace Senga amefanya baraza na askari wa Mkoa wa Songwe Januari 03, 2025 katika ukumbi wa Polisi uliyopo Vwawa Wilaya ya Mbozi na kuwataka askari hao kuendelea kutekeleza jukumu mama la kulinda raia na mali zao ikiwa ni pamoja na kuzuia uhalifu ili kuleta maendeleo kwenye Jamii.

Kamanda Senga aliwasisitiza askari hao kufanya kazi kwa kuzingatia Nidhamu, Haki, Weledi na Uadilifu na kutenda kwa kuzingatia sheria za nchi bila kumuonea mtu na kutokuwa na muhali kwa wahalifu.

Naye, Afisa Mnadhimu wa Polisi Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Akama Shaaban aliwataka askari hao kuwapa elimu wananchi wanaofungua kesi kufika mahakamani kwa lengo la kutoa ushahidi ili kuweza kupata mafanikio ya kesi hizo na iwe fundisho kwa jamii.

Kwa upande wake Mkuu wa Operesheni Mkoa wa Songwe (ACP) Nicholas Livingstone aliwasisitiza Askari hao kufanya doria na misako yenye tija ili ilete mafanikio ikiwa ni pamoja na kuendelea kujenga umoja na ushirikiano kwa wananchi kwa lengo la kupata taarifa za uhalifu na wahalifu katika jamii.






Related Posts