Na Humphrey Shao, Michuzi tv
Kituo kipya cha Afya cha The Cure Specialized Polyclinic kimeziduliwa rasmi leo na papo hapo kusema, kimeajiandaa kuweka kambi maalum ya kutoa huduma za vipimo na matibabu katika kushiriki siku ya Kansa Duniani itakayoadhimishwa mwezi ujao wa Februari mwaka huu.
Kituo hicho kimesema, kwenye kambi hiyo, kitatoa chanjo ya Saratani ya kizazi, elimu kuhusu masuala ya ujauzito (preginancy Awareness), elimu na huduma kuhusu magonjwa ya zinaa/ya kuambukiza, kutoa huduma za kiganga na kuelimisha kuhusu mtindo wa maisha (Health Lifestyle awareness).
Hayo yamesemwa na Mmoja wa Wakurugenzi wa The Cure Specialized Polyclinic Dk. (PhD) Rehema Idriss Mzimbiri, akizungumza wakati wa Uzinduzi rasmi wa Kituo hicho uliofanyika leo Jumamosi, januari 4, 2025, nje kidogo ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Upanga Jijini Dar es Salaam.
“Kuelekea mwezi Februari kwa kalenda ya Afya ya Dunia, The Cure Specialized Polyclinic tunategemea kuweka kambi maalum ya kuadhimisha Siku ya Kansa Duniani (Cancer Worl Day), Kuelimisha kuhusu masuala ya ujauzito, kutoa elimu na huduma zinazohusiana na majongwa ya zinaa/ya kuambukiza, kelimisha kuhusu mtindo wa maisha (Health Lifestyle awareness) na kutoa chanjo ya Saratani ya kizazi.” alisema Dk. (PhD) Rehema.
Kuhusu dhima ya kuanzisha kituo hicho, Dk. (PhD) Rehema alisema, kaulimbiu ya The Cure Specialized Polyclinic ni kutoa huduma bora, Afya Endelevu, Ustawi wa kila mtu na kwamba kaulimbiu hiyo inaakisi dhamira yao ya kutoa huduma za afya bora na endelevu kwa wateja wakw huku kikizingatia mahitaji ya wateja hao na kuhakikisha ustawi wao wa muda mrefu.
” Lengo letu ni kuhakikisha kila mtu anapata huduma bora za afya, zinazofaa, na zinazodumu. katika The Cure Specialized Polyclinic tumejizatiti kuwa kituo cha afya kinachotoa kinachotoa huduma za kisasa na zenye ufanisi mkubwa”. alisema Dk. (PhD) Rehema na kutaja huduma ambazo kituo hicho kitato kuwa ni pamoja na;
1. Ushauri wa Wataalam wa afya, ikiwa ni pamoja na daktari bingwa na bobezi ambapo itahusisha huduma ya kitaalam inayotolewa na wataalam wenye ujuzi katika maeneo maalum ya matibabu.
2. Vipimo vya maabara na radiolojia vya kisasa, akisema vipimo hivyo ni pamoja na uchunguzi wa sampuli z damu, ECHO, kugundua matatizo kama ya magonjwa ya Vaivu, ufanisi wa moyo, na EEG (umeme wa ubongo na ULTRA SOUND, Huduma ya CT Scan, MRI na X-ray.
3. Tiba ya mazoezi-tiba (physiotherapy) kwa wahitaji ambayo alisema ni matibau ya mazoezi kwa kutumia mbinu mbalimbali kama za mikono na vifaa vya kisasa ambavyo husaidia kurekebisha na kunoresha hali za mgonjwa hasa katika mifupa, misuli, viungo na mfumo wa neva.
4. Huduma za kisaikolojia ambazo ni za kitaalam kwa wanaokutana na changamoto za kiakili, kihisia na kisaikolojia.
5.Huduma za lishe ambazo zinahusisha ushauri wa mlo bora, mipango ya lishe kwa wagonjwa maalum, elimu kuhusu virutubisho, na msaada wa kubadilisha tabia za lishe. Husaidia kuboresha afya , kudhibiti magonjwa na kukuza ustawi wa kimwili na kiakili.
“The Cure Specialized Polyclinic tunajivunia kuwa na timu ya wataalamu wa afya wenye ujuzi na uzoefu ambao watahakikisha kila mteja anapata huduma bora katika maisha ya kila siku. Kituo hiki kinatambua umuhimu wa afya bora katika maisha ya kila mtu, na tunajitahidi kutoa huduma ambazo zitasaidia kukuza ustawi wa jamii yetu”, alisema Dk. (PhD) Rehema.
Akizungumza mwishoni mwa hafla hiyo, Mkurugenzi wa The Cure Specialized Polyclinic Dk. Juma Magogo Mzimbiri, alisema kituo hicho kina uwezo wa kupokea wagonjwa hadi 50 kwa siku.
‘Wanafamilia’ wakizindua Kituo kipya cha Afya cha The Cure Specialized Polyclinic, hatua chache kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, eneo la Upanga Jijini Dar es Salaam, leo Jumamosi, Januari 4, 2025. Kulia ni Mmoja wa Wakurugenzi wa The Cure Specialized Polyclinic Dk. (PhD) Rehema Idriss Mzimbiri na wapili ni Mkurugenzi wa Kituo hicho Dk. Juma Magogo Mzimbiri na Dk. Hamisa Iddy Khamis.
Dk. Hamisa Iddy Khamis akitoa utangulizi na utambulisho wakati wa uzinduzi wa kituo hicho.
Baadhi ya Wawalikwa wakiwa kwenye uzinduzi wa Kituo hicho.
Wafafamilia wa Mzimbiri wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa kituo hicho. Kushoto ni baadhi ya waalikwa.
Wafafamilia wa Mzimbiri wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa kituo hicho
Dk. PhD Rehema akisoma hutuba ya uzinduzi wa kituo hicho.
Dk. PhD Rehema akisoma hutuba ya uzinduzi wa kituo hicho.
Baadhi ya Wawalikwa wakimsikiliza Dk. (PhD) kwenye uzinduzi wa Kituo hicho.
Dk. (PhD) akipongezwa na Dk. Hamisa baada ya hotuba yake.
Wanafamilia wakifanya uzinduzi wa kituo hicho.
Baadhi ya Waalikwa na watumishi wa kituo hicho wakishangilia uzinduzi.
WAALIKWA WAKIONYESHWA VIFAA KATIKA KITUO HICHO
Dk. Mzimbiri akitoa neno la shukurani mwishoni mwa uzinduzi wa kituo hicho..