Wabongo nguvu sawa Uturuki | Mwanaspoti

BAADA ya tambo za Watanzania wawili wanaokipiga katika Ligi ya Walemavu nchini Uturuki hatimaye mechi baina ya timu zao imemalizika kwa sare ya 1-1.

Nyota hao ni Hebron Shedrack wa Sisli Yeditepe na Ramadhan Chomelo anayekipiga Konya Amputee ambao walikutana kwenye mchezo wa Ligi hiyo uliojaa ushindani.

Akizungumza na Mwanaspoti, Shedrack ambaye pia aliifunga timu ya Chomelo alisema imekuwa kawaida kwake kumfunga Mbongo mwenzake kila wanapokutana kwenye mchezo unaowakutanisha wawili hao.

“Hii ni mara ya tatu naifunga Konya kila tunapokutana, ni taswira nzuri kutokana na ninapocheza na Mtanzania mwenzangu ikatokea mmoja kashinda ni jambo jema na tuna tengeneza milango kwa wenzetu kutokana tunapocheza wanajua kuwa Tanzania kuna vipaji,” alisema Shedrack.

Kwa upande wa Chomelo alisema ingawa nyota mwenzake amelifunga chama lake lakini ni furaha kwa kuwa wametoka sare.

“Ingekuwa tabu kama wangetufunga, yeye ndio aliifungia timu yake lakini kwenye timu yangu mimi ndo nilitoa pre assist lakini ni furaha tunapokutana ukiachana na ushindani wa uwanjani ni marafiki sana.”

Related Posts