Mtangazaji aliyedaiwa kupotea apatikana kwa shangazi yake Kitunda

Dar es Salam. Mtangazaji wa TV 3, Gwamaka Francis Gehas, mkazi wa Mbezi Beach African, Dar es Salaam aliyedaiwa kupotea Januari 3, 2025  amepatikana akiwa kwa shangazi yake Kitunda.

Kwa mujibu wa taarifa ya Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime iliyotolewa jana Januari 5, Makao Makuu ya Polisi Dodoma, imebainisha kuwa baada ya ufuatiliaji ulioanza kwa kukusanya ushahidi na taarifa kutoka kwa watu mbalimbali,jana walipokea taarifa kuwa Gwamaka yupo Kitunda nyumbani kwa shangazi yake.

Aidha, Jeshi la Polisi limesema linaendelea na uchunguzi, ikiwa ni pamoja na kupata maelezo yake ili kujua uhalisia wa tukio la kutokuonekana kwake na baadaye kuonekana akiwa kwa shangazi yake.

“Uchunguzi huu utatusaidia kupata ukweli kuna kitu gani nyuma yake, ili hatua stahiki zichukuliwe kulingana na ushahidi utakaopatikana,” imeeleza taarifa hiyo.

Endelea kufuatilia Mwananchi.

Related Posts