Mashujaa Yabeba wawili Yanga SC

WAPINZANI wa Yanga Princess katika Ligi ya Wanawake, Mashujaa Queens yenye maskani yake jijini Dar es Salaam imesajili wachezaji wawili kwa mkopo kutoka kwa wananchi hao.

Timu hiyo imemaliza duru la kwanza ikiwa katika nafasi ya tatu kwenye msimamo kwa pointi 15 ikiishusha Yanga iliyopo nafasi ya nne ikiwa na pointi 12 baada ya kucheza michezo minane.

Mwanaspoti ilipomtafuta Mratibu wa Yanga, Kibwana Matokeo alisema wamewatoa kwa mkopo wachezaji wawili straika Annastazia Shau na beki Masika Mwakisua ambao wamekuwa wakicheza muda mchache.

“Ndio tumetoa wachezaji wawili ambao Mashujaa iliomba kuwa nao kwa mkopo wa miezi sita, kama viongozi tumeona tuwaachie kwa sababu wamekuwa wakicheza muda mchache hivyo tukatoa fursa waende kupata muda mwingi wa kucheza,” alisema Matokeo.

Baada ya kutambulishwa Mashujaa straika huyo mchezo wake wa kwanza dhidi ya Mlandizi Queens akafunga hat-trick akiingia kwenye kitabu cha vinara wa mabao wa ligi hiyo ya wanawake.

Related Posts