Wanafunzi 86 St. Anne Marie Academy wachaguliwa shule za vipaji maalum

 

WANAFUNZI 86 kati ya 156 wa shule ya St Anne Marie Academy ya Mbezi Kimara kwa Msuguri jijini Dar es Salaam waliohitimu darasa la saba wamechaguliwa kujiunga na shule za vipaji maalum. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mkuu wa shule hiyo, Komredi Gladius Ndyetabula alisema jana kuwa wanafunzi wote wa shule hiyo waliohitimu darasa la sana 2024 walipata alama A.

Alisema wamefurahi kuona zaidi ya asilimia 55 ya wahitimu wa darasa la saba wanachaguliwa kujiunga na shule za vipaji maalum huku akitaja siri ya mafanikio hayo kuwa ni uwekezaji mkubwa uliofanywa na Mkurugenzi wa shule hizo.

Ndyetabula alisema Mkurugenzi wa shule hizo, ambaye ni Mbunge wa Bukoba Vijijini (CCM), Dk. Jasson Rweikiza ameweka mazingira mazuri ya shule hiyo zikiwemo maktaba za kisasa zilizosheheni vitabu vya kutosha na mifumo ya ufuatiliaji matokeo ya mitihani ndani ya shule hiyo.

Alisema hata kwenye matokeo ya darasa la nne yaliyotangazwa na Baraza la Mitihani NECTA mwishoni mwa wiki, wanafunzi 100 wa shule hiyo kati ya 174 wamepata alama A na waliobaki 74 walipata alama B.

“Kwa upande wa matokeo ya kidato cha pili shule wanafunzi 60 wamepata division one, wanafunzi 26 daraja la pili na wanafunzi 31 daraja la tatu, kidato cha sita mwaka 2024 tulikuwa na wanafunzi 48 daraja la kwanza, daraja la pili wanafunzi 86 na daraja la tatu wanafunzi 24,” alisema

“Shule hii imekuwa ndani ya 10 bora kitaifa miaka mingi na mwaka 2021 ilitoa mwanafunzi bora kitaifa kwenye matokeo ya darasa la saba, tuna huduma nzuri sana kuanzia mabweni, mashamba ya mboga mboga, maktaba na maabara za kisasa, walimu wa kutosha na wenye weledi wa hali ya juu sana,” alisema

Alisema shule hiyo inafundisha lugha ya Kifaransa na wanafunzi wengi wamefanikiwa kuimudu lugha hiyo akisema kuwa wako mbioni kuanza kufundisha lugha ya kichina shuleni hapo.

About The Author

Related Posts