Mbeto : ACT kitazusha uongo hakitashinda uchaguzi Zanzibar


Na Mwandishi Maalum , Zanziabr

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema baada ya ACT Wazalendo kuishiwa hoja za kuwaaeleza wananchi kitazua uongo na upotoshaji lakini hakina ubavu wa kushinda urais katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka

CCM kimesisitiza ACT toka sasa hadi oktoba mwaka huu ,viongozi wake watapayuka sana kutokana na haiba iliopo ya ustawi wa maendeleo yalioimarika Zanzibar.

Ufafanuzi huo umetolewa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Idara ya Itikadi,Uenezi na Mafunzo ,Khamisi Mbeto Khamis ,aliyesema kazi ya utafiti na uchimbaji mafuta ilianza baada ya michakato yote kukamilika kwa mujibu wa sheria.

Mbeto alisema hakuna kiongozi yeyote wa ACT mwenye ubavu wa kukwamisha uamuzi wa Serikali isifikie maamuzi yake ya kuchimba mafuta kwa manufaa na maslahi ya nchi na wananchi .

Alisema pia hawawezi kukwamisha mpango wa uchimbaji wa mafuta na gesi asilia kwasababu smz imeshachukua hatua zote muhimu za kuanza mradi wa uchimbaji mafuta.

Alieleza katika serikali ya awamu ya saba chini ya Rais mstaafu Dkt Ali Mohamed shein , ilipitishwa sheria Namba 6 ya Mwaka 2016 ya Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia, wakiwemo Wawakikishi na Mawaziri toka upinzani .

Pia Mbeto aliongeza kusema Mwaka 2017 chini ya Rais Dk Shein,SMZ ilianzisha Shirika la Maendeleo ya Petroli Zanzibar ( ZPDC) na mwaka huo huo Mamlaka ya Usimamizi na Utafutaji wa Mafuta na Gesi Asilia( ZPRA) ikaanzishwa.

“ACT Wazalendo nilishasema kuanzia sasa kuelekea oktoba mwaka huu viongozi wake wataropoka meneno mengi kuthibisha wana mradi wa siasa chafu .Wameishiwa maneno ya kuwaeleza wananchi na sasa wanazidi kupuuzwa ” Alisema Mbeto

Akifafanua zaidi ,Mbeto alisema kazi ya utafutaji Mafuta na Gesi Asilia ilianza rasmi mwaka 2017 kwa njia ya mitetemo, Angani na Baharini ambapo Kampuni ya Rak Gas ya Ras Kheimah ya Falme za Kiarabu – UAE ilianza kazi hiyo na kukamilika mwaka 2019 kwa Kitalu Namba 9 cha Pemba- Zanzibar.

Aidha Mwaka 2019, SMZ ilisaini Mkataba wa Mgawanyo wa Rasilimali ya Mafuta na Gesi Asilia (PSA) na Kampuni ya Rak Gas bila kuwepo mivutano ,migongano wala matatizo yoyote .

Akikizungumzia Kitalu cha Pemba – Zanzibar, alisema kimsingi Kitalu hicho pia kimegusa maeneo ya Mkoa wa Tanga, lakini kwa kuwa Zanzibar ni sehemu ya Tanzania, Serikali ya muungano imeachia Zanzibar.

Mbeto alimtaja aliyekuwa Waziri wa Habari toka upinzani katika awamu ya saba , Said Ali Mbarouk, aliwahi kuingia mkataba mbovu na Kampuni ya AGAPE kuhusu Ving’amuzi vya runinga na kuitia hasara kubwa SMZ

Akimzungmzia Mjumbe wa Kamati kuu ya ACT Mansour Yussuf Himid ,Mbeto alimtaka Mwanasiasa huyo ni vema angefunga mdomo wake ,akae kimya kwani akiwa Waziri smz hakuwa kiongozi mzalendo .

Mbeto alisema Mansour akiwa Waziri hakufanya lolote lililoleta manufaa hususan katika suala la Mafuta na Gesi zaidi ya kukosa nidhamu kwa viongozi wake hadi akafukuzwa Uwaziri na kuvuliwa uanachama CCM.

 

Related Posts