_Asisitiza kuboresha huduma kwa Wateja na usimamizi thabiti ya huduma ya Majisafi
Naibu Waziri wa Maji Mhe. Kundo Andrea Mathew (Mb) ameanza ziara ya kikazi ya siku mbili katika Mkoa wa Pwani yenye lengo la kuangalia njia bora za kuboresha huduma ya maji katika Mkoa huo.
Mhe.Kundo ameeleza dhumuni ya ziara yake ni kukutana wa wataalamu wa Sekta ya maji Mkoa wa Pwani na kukumbushana wajibu wao kwa Wananchi wanaowahudumia, pia kuboresha huduma kwa wateja na kuelezea utekelezaji miradi ya Majisafi na Usafi wa Mazingira iliyotekelezwa na Serikali kwa Wananchi.
“Tupo hapa kuhakikisha maelekezo ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan yanatekelezwa lakini pia kuhakikisha ilani ya Chama inatekelezwa ipasavyo. Tukumbuke kuwa ni haki ya Mwananchi kupata huduma ya majisafi na salama lakini pia kupata taarifa sahihi na kwa wakati endapo kumetokea upungufu wa huduma” ameeleza Mhe.Kundo.
Mhandisi Kundo ameongeza kuwa Mkoa wa Pwani awali upatikanaji wa huduma ya maji ilikuwa asilimia 59 (2020) na kwa awamu ya Sita upatikanaji wa huduma umeongezeka na kufikia asilimia zaidi ya 86 (2024).
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe.Abubakari Kunenge amemshukuru Waziri wa Maji Kwa ziara yake kwani itasaidia kuboresha huduma ya maji katika Mkoa huu na kufikia dhima ya Mh.Rais ya Kumtua mama ndoo ya maji kichwani.
“Mkoa wetu, ni Mkoa wa Viwanda, lakini makazi ya watu pia yanakua kwa Kasi kubwa, haya yote yanahitaji huduma bora ya maji, ujio wako leo utaleta matokeo chanya kwani tunategemea huduma ya maji inaenda kuimarika zaidi mkoni kwetu.