Makamu wa Rais Dk.Mpango aipongeza shule ya Istiqaama ya Tanga kwa Usafi

 Na Barnabas Lugwisha

Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungani wa Tanzania amezindua awamu ya pili ya Pili ya kampeni ya ‘Mtu ni afya ‘juzi Mjini Kibaha Mkoa wa Pwami ikiwa ni mara ya 50 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1973. 

Na katika hafla hiyo Shule ya Istiqaama ya Jijini Tanga ilishika nafasi ya pili katika Mshindano ya Afya na Usafi wa Mazingira kundi la shule za Sekondari Tanzania Bara.

Dk Mpango alisisitiza umuhimu wa kutunza Mazingira na kuendelea kuzingatia kanuni za afya, makamu wa Rais amezipongeza taasisi ambazo zimefanya vizuri katika swala la afya na usafi wa mazingira ambao kwenye kundi la shule za Sekondari Tanzania Bara ameipongeza shule ya Istiqaama ya Jijini Tanga kwa kushika nafasi ya Pili shule zilizofanya vizuri zaidi kwa mwaka 2023.

Kwa Upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Mohamed Hamad Mohamed ameupokea ushindi huo kwa furaha na kuahidi kufanya vizuri zaidi kwa mwaka unaokuja.“Kwa upende wetu usihindi huu ni chachu ya kufanya vizuri zaidi katika mashindano yajayo.

 Mwalimu Mkuu wa Shule ya Istiqaama ya Jijini Tanga Mohamed Hamad Mohamed (kushoto) akiwa na Msimamizi wa Shule hiyo Ahmed Abdalah baada ya kutunukiwa Cheti cha nafasi ya pili katika Mshindano ya Afya na Usafi wa Mazingira kundi la shule za Sekondari Tanzania Bara,  hafla iliyofanyika Kibaha Mkoani Pwani.

Msimamizi wa Shule ya sekondari ya Istiqaama Ahmed Abdalah  ya Jijini Tanga (kushoto)  akiwa na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu (katikati) mara baada ya kutunukiwa cheti cha nafasi ya pili katika Mshindano ya Afya na Usafi wa Mazingira kundi la shule za Sekondari Tanzania Bara, kulia ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Mohamed Hamad Mohamed  

Related Posts