MISS HIGHER LEARNING YAFUNGUA DIRISHA LA USAHILI WAREMBO VYUONI WAPEWA SHAVU

MKURUGENZI wa “The Look ” Kampuni inayoendesha Mashirikiano ya Miss Tanzania, Basilla Mwanukuzi amesema kupitia shindano la Urembo kupita ngazi ya vyuo vikuu (MISS HIGHER LEARNING) limekuwa likiacha alama nzuri kwani mara 3 mfululizo limekuwa likitoa washiriki katika ngazi hiyo na kufanikisha Miss Tanzania hadi kufika Miss World .

Ameyasema hayo Mei 11,2024 Jijini Dar es Salaam, wakati wa ufunguzi wa shindano hilo, na kusema kuwa anatambua kuwa urembo ni uongozi lakini haitoshi kukamilisha sifa za mrembo huyo ni lazima awe na ufahamu mzuri .

“Miss Tanzania 2023 ametokea ngazi ya vyuo vikuu hivyo ni kielelezo tosha kuwa Miss Higher Learning inatoa Warembo wasomi ambao wanaandaliwa kuja kusaidia jamii na Taifa kwa ujumla”. Amesema

Pia ameongeza kuwa jukwaa la Miss Tanzania limekuwa ni msaada mkubwa kwa sasa kuwatumia warembo katika nyanja mbalimbali ikiwemo kisiasa,sanaa pamoja na kijamii na Makampuni ili kusaidia kufanikisha lengo au kusudio la jambo lolote la Kimaendeleo .

Kwa upande wake Mwanzilishi wa Shindano hilo Adam Kundiya amesema shindano la mwaka huu litakuwa na Kipaumbele zaidi kutokana na alama iliyowekwa na Miss Tanzania 2023 Trace Nabukera na warembo wengine ambao walifika mchujo wa mwisho (Top 5).

Aidha ameeleza kuwa usahili utaanza rasmi Mei 25,2024 Katika Mgahawa wa Hug Mug Masaki Jijini Dar es Salaam ambapo amefafanua zaidi kuwa sifa za ushiriki ni kuwa na umri kuanzia miaka 18 hadi 23 ambapo kwa Wanafunzi waliomaliza 2022,2023,2024 nafasi imetokea kwa mwaka huu.

Naye Mdhamini mpya wa shindano hilo kutoka Benki ya DTB Afisa uwezeshaji Dennis Rauya amesema kupitia benki hiyo imeingia rasmi kwenye mashindano hayo ili kumpa rasilimali fedha mrembo kuhakikisha anatumia fedha kutimiza project yake ambayo katika mashindano hayo ndio kielelezo tosha cha kumpeleka Mrembo kuingia katika kinyang’anyiro cha Miss Tanzania hadi kushiriki Miss world.

Mkurugenzi wa Kampuni ya “The Look” Basilla Mwanukuzi akizungumza na Wanahabari Leo Mei 11,2024 Masaki Jijini Dar es Salaam mara baada ya kufungua rasmi Shindano la Urembo la ngazi ya Vyuo Vikuu (MISS HIGHER LEARNING) Kwa Msimu mwengine ambapo amesema Warembo wanaotoka vyuoni wana mchango mkubwa katika Jukwaa la urembo na kuwataka warembo hao kutumia jukwaa hilo vizuri ili waendelee kutumiwa kama kielelezo cha Mafanikio katika nyanja zote
 

Mkurugenzi wa Kampuni ya Kundyakraft Adam Kundiya  akikabidhi zawadi kwa Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Kampuni ya “The Look ” Basilla kutoka kwa “Prima Afro” kwa Meneja masoko  Novacutus mara baada ya ufunguzi wa Mashindano ya Miss higher Learning msimu wa tatu

Related Posts