UCHUMI WA TANZANIA UNATARAJIWA KUKUA KWA ASILIMIA 5.7 KATIKA ROBO YA NNE YA MWAKA 2024

NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV

UCHUMI wa Tanzania Bara na Zanzibar umeendelea kuwa imara kwa mwaka 2024 ambapo Uchumi wa Tanzania Bara ulikua kwa asilimia 5.4 katika nusu ya kwanza ya mwaka 2024, na unatarajiwa kukua kwa asilimia 5.6 katika robo ya tatu na asilimia 5.7 katika robo ya nne ya mwaka 2024.  

Kwa kuzingatia mwenendo huo, ukuaji wa uchumi unatarajiwa kuwa sawia na matokeo ya ukuaji wa asilimia 5.4 kwa mwaka 2024.

Hayo yameelezwa leo Januari 8, 2025 na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Emmanuel Tutuba wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kikao cha robo mwaka cha Kamati ya Sera ya Fedha ya Benki Kuu ya Tanzania kufanyika na kufanya tathmini ya mwenendo wa hali ya uchumi wa dunia na hapa nchini.

Amesema ukuaji huu umechangiwa zaidi na ongezeko la shughuli za kilimo, usafirishaji, ujenzi, na biashara ambapo kwa upande wa Zanzibar, uchumi ulikua kwa asilimia 6.8 katika robo ya kwanza na asilimia 7.2 katika robo ya pili ya mwaka 2024, na unakadiriwa kukua kwa viwango hivyo kwa robo mbili zinazofuata, hivyo kufikia maoteo ya ukuaji wa asilimia 7.2 kwa mwaka 2024. 

Aidha Tutuba amesema katika mwaka 2025, ukuaji wa uchumi kwa Tanzania Bara na Zanzibar unatarajiwa kuendelea kuwa wa kasi ya kuridhisha, kwa takriban asilimia 6 na asilimia 6.8, mtawalia. 

“Ukuaji huu unatarajiwa kuchangiwa na ongezeko la uzalishaji katika shughuli za kilimo, utekelezaji wa miradi ya ujenzi, maboresho katika usafirishaji na ugavi, nishati ya uhakika, pamoja na utekelezaji wa sera za fedha na kibajeti”. Amesema 

Amesema mfumuko wa bei uliendelea kuwa tulivu katika kipindi chote cha mwaka 2024, ukiwa chini ya lengo la asilimia 5 kwa Tanzania Bara na kukaribia lengo hilo kwa upande wa Zanzibar. 

Tutuba amesema katika robo ya nne ya mwaka 2024, mfumuko wa bei kwa Tanzania Bara ulikuwa wastani wa asilimia 3 kutokana na upatikanaji wa chakula cha kutosha, utekelezaji wa sera thabiti za fedha na bajeti, na kupungua kwa bei za bidhaa katika soko la dunia, hususan mafuta ghafi. 

Vilevile amesema kwa upande wa Zanzibar, mfumuko wa bei ulipungua hadi asilimia 4.5 mwezi Novemba 2024.

“Mfumuko wa bei unatarajiwa kuendelea kuwa tulivu katika robo ya kwanza ya mwaka 2025, ukibakia katika viwango vya kati ya asilimia 3.1 na asilimia 4.  Hali hii itatokana na kuendelea kuwepo kwa chakula cha kutosha, utulivu wa thamani ya shilingi dhidi ya fedha za kigeni, umeme wa uhakika, na kushuka kwa bei za bidhaa katika soko la dunia, hususan mafuta ghafi. 

Pamoja na hayo Gavana Tutuba amesema thamani ya shilingi inatarajiwa kuwa imara katika robo ya kwanza ya mwaka 2025, kutokana na kuwepo kwa ukwasi wa kutosha wa fedha za kigeni uliopatikana katika robo ya nne ya mwaka 2024, utekelezaji wa sera ya fedha kutokana, uamuzi wa kubakiza Riba ya Benki Kuu kuwa asilimia 6, na bei za bidhaa katika soko la dunia kuwa nafuu.

Amesema Benki Kuu inatarajia kuendelea kuwa na akiba ya kutosha ya fedha za kigeni, na kuongeza fedha za kigeni pale itapohitajika. Akiba iliyopo sasa ni zaidi ya dola za Marekani bilioni 5.5, kiwango ambacho kinatosheleza uagizaji wa bidhaa na huduma kutoka nje kwa zaidi ya miezi 4.7.

“Akiba hiyo inatarajiwa kubaki katika kiwango hicho katika robo ya kwanza ya mwaka 2025 kutokana na juhudi zinazofanywa na Benki kuu katika kuongeza akiba ya fedha za kigeni, ikiwemo kununua dhahabu hapa nchini”. Ameeleza Gavana Tutuba.

Sanjari na hayo amesema deni la Taifa liliendelea kuwa himilivu, ambapo kwa mwaka 2023/24 lilikuwa takriban asilimia 41.1 ya Pato la Taifa (GDP) kwa thamani halisi ya sasa (NPV). 

Kiwango hiki kilikua chini ya ukomo wa uhimilivu wa nchi na kigezo cha mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) cha asilimia 55 na asilimia 50, mtawalia”.  Amesema

Amesema kwa kuzingatia thamani ya bei za sasa, deni la Taifa lilikuwa asilimia 46.1 ya Pato la Taifa, chini ya kigezo cha mtangamano kwa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) cha ukomo wa asilimia 60.

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Emmanuel Tutuba akiwasilisha mrejesho wa kikao cha Kamati ya Sera ya Fedha (MPC) ya Benki Kuu ya Tanzania kwa Wakuu wa Taasisi za kifedha nchini ambayo ilifanya kikao chake cha kila robo mwaka Januari 7, 2025 na kufanya tathmini ya mwenendo wa hali ya uchumi wa dunia na hapa nchini. Tukio hilo limefanyika leo Januari 8, 2024 katika Ofisi za Benki Kuu ya Tanzania Jijini Dar es Salaam.

Wakuu wa Taasisi za Kifedha nchini wakipata mrejesho wa kikao cha Kamati ya Sera ya Fedha (MPC) ya Benki Kuu ya Tanzania ambayo ilifanya kikao chake cha kila robo mwaka Januari 7, 2025 na kufanya tathmini ya mwenendo wa hali ya uchumi wa dunia na hapa nchini. Tukio hilo limefanyika leo Januari 8, 2024 katika Ofisi za Benki Kuu ya Tanzania Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Related Posts