Paris Hilton ni miongoni mwa mastaa ambao wamekumbwa na athari za moja kwa moja kufuatia moto mkubwa unaoendelea kuwaka Los Angeles nchini Marekani ambapo moja kati ya nyumba zake iliyopo Malibu kando ya bahari, imeteketea kwa moto.
TMZ imeeleza kuwa nyumba hiyo imeteketea yote baada ya kupitiwa na moto huo unaochochewa na upepo mkali.
Taarifa zaidi zinaeleza kuwa, licha ya nyumba hiyo kuteketea, Paris Hilton bado anayo mijengo mingine kibao likiwemo jumba la kifahari lililopo Beverly Hills.
Hilton amenukuliwa akisema aliishuhudia nyumba yake hiyo ikiteketea kwenye picha za video alizoziona kwenye televisheni.
“Nilikuwa nimekaa na familia yangu tukitazama habari kwenye runinga, mara tukashuhudia nyumba yetu ikiteketea! Ni jambo lililotushtua na kutuhuzunisha sana,” aliandika kwenye akaunti yake ya Instagram.