Evarist aongoza tena kwa kutupia

MCHEZAJI Davidson Evarist wa timu ya Christ the King, bado anaendelea kutesa kwa ufungaji katika Ligi Daraja la Kwanza Mkoa wa Dar es Salaam, baada ya kufunga pointi 342.

Staa huyo anafuatiwa na Fahmi Hamad, kutoka timu ya Polisi aliyefunga pointi 252, huku Diocres Mugoba wa timu ya Premier Academy akishika nafasi ya tatu kwa pointi 247.

Wachezaji wengine waliofuatia ni George Mwakyanjala (Yellow Jacket) pointi 212, Ally Songoro (Magone) 197 na Lawi Mwambasi (Polisi) 197.

Wengine ni Jackson Mrisho (Mbezi Beach) pointi 190, Martine Rodgers (Mlimani  B.C) 187, Dickson Thomas (Kigamboni) 184 na Adam Ramadhani (Mbezi Beach) 172.

Davis Msham wa timu ya Stein Warriors anaongoza kwa kutoa “asisti” mara 53,  katika ligi ya Daraja la Kwanza ya Mkoa wa Dar es Salaam, akifuatiwa na Issa Ismail wa Polisi aliyetoa mara 41.

Wachezaji wengine ni Haykal Ibrahim (Kurasini Heat), aliyetoa asisti mara 40, Jacob Marenga (Chang’ombe) 39, Ally Songoro (Magone) 38.

Wengine ni Omary Njota (Yellow Jacket) 36 Gabriel Gilbert (Yellow Jacket) 36, Robert Mwaipungu (Christ the King), Brandom Odhuno (Chang’ombe) 34 na Lawi Mwambasi (Polisi) 34.

Mchezaji Lawi Mwambasi wa timu ya  Polisi anaongoza kwa kudaka mipira iliyoridi (rebound) mara 141, katika ligi hiyo.

Wanaofuatia ni Wilson Maketa wa timu ya Mbezi Beach aliyedaka  mara 140, Hillary Ferix  (Kurasini Heat) 113, Denis Jomalema (Magnet) 107, Abuu Hassan (Kibada Riders) 105.

Wengine ni Lawrence James (Dar King) mara 105, Farmi Hamad (Polisi) 103, Emaunel Mwikalo (Yellow Jacket) 91 na Berry Kankonde (Chang’ombe) 85 na Francis Mallya (82).

Related Posts