Dar es Salaam. Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema wanamshikilia aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chadema na balozi wa Tanzania nchini Sweden, Dk Wilbrod Slaa.
Kamanda Muliro amethibitisha hayo leo Ijumaa Januari 10, 2024 kupitia kipindi cha Good Morning cha Wasafi.
“Daktari yupo, tuko naye na tumekuwa na mahojiano naye kwa baadhi ya mambo na yanakwenda vizuri kwa hiyo tunaiangalia mifumo ya kisheria inatuelekeza ni nini cha kufanya na taarifa kamili zitatolewa baadaye,” amesema Kamanda Muliro.
Taarifa ya kukamatwa kwa Dk Slaa imesambaa kupitia mitandao ya kijamii, ikisikika sauti ya mwanasiasa huyo akizungumza kuhusu kukamatwa na Jeshi la Polisi na kwamba anapelekwa katika Kituo cha Polisi cha Mbweni, Dar es Salaam.
Endelea kufuatilia Mwananchi.