Makamu wa Pili Mstaafu wa awamu ya saba wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewataka Mahakimu na Majaji kufanya kazi kwa uadilifu wanapo sikiliza mashauri ya wananchi.
Ameyasema hayo huko Binguni Mkoa wa Kusini Unguja wakati akiweka jiwe la msingi Mahkama ya Mkoa wa Kusini kufuatia shamrashamra za kuadhimisha miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Amesema Mahkama si pahali pa uonevu ni sehemu ya upatikanaji haki kwani wananchi wanapo kwenda mahkamani hujihakikishia kuwa wanakwenda katika eneo la kupata haki zao hivyo inapotokea hakimu hafanyi uadilifu anakwenda kinyume taratibu za upatikanaji wa haki.
Aidha amewataka wananchi wasichukue Sheria mikononi mwao kwa kuwapa kesi watu wasio na hatia kwani wanakwenda kinyume na Sheria za nchi, sambamba na kwenda Mahkamani kutoa ushahidi kwani haki haitopatikana bila ya kuwepo ushahidi imara.
Hatahivyo amewataka Viongozi wa Mahkama kusimamia majengo hayo yanayo zinduliwa na kuwekewa jiwe la msingi ili yaweze kudumu kwa muda mrefu na kutumika kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
Akitoa taarifa ya kitaalamu Mtendaji Mkuu wa Mahkama Kai Bashir Mbarouk amesema ujenzi wa Mahkama hiyo umekuja baada ya kuona baadhi ya uchakavu wa majengo ya Mahkama walizokuwa wakifanyia kazi na kutotosha kwa nafasi za kufanyia kazi.
Alisema awamu ya kwanza watajenga majengo saba na awamu ya pili watajenga saba ambapo majengo hayo ya tajengwa kwa kila Mikoa na Wilaya Unguja na Pemba.
Kwa upande wake Jaji Mkuu wa Zanzibar Khamis Ramadhan Abdalla aamesema kuwa kuwepo kwa Mahkama hiyo kutatua changamoto ya wafuata huduma katika masafa marefu kwa wananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja ambapo lengo la ujenzi huo utahakikisha wananchi wanapata huduma za Mahkama katika maeneo ya karibu.
Ujenzi huo utakamilika kwa miezi 12 ukisimamiwa na Kampuni ya Hub Consultancy kutoka Dar es_salam na kujengwa na Kampuni ya CRJE kutoka China.
Makamu wa Pili wa Rais Mstaafu Balozi Seif Ali Idi
(kulia)akikunjuwa Kitambaa kuashiria Uwekaji wa Jiwe la Msingi Mahkama
ya Mkoa wa Kusini Bungi Wilaya ya Kati Zanzibar.Ikiwa ni Katika Shamra
shamra za maika 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar,yenye kauli mbiu “Miaka 61
ya Mapinduzi :Amani ,Umoja na Mshikamano kwa Maendeleo yetu.
Makamu wa Pili wa Rais Mstaafu Balozi Seif Ali Idi akipatiwa
Maelezo na Msanifu Majengo Mahkama Kuu Awena Keis kuhusiana na Ujenzi
ulivyoanza katika hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi Mahkama ya Mkoa wa
Kusini Bungi Wilaya ya Kati Unguja.Ikiwa ni Katika Shamra shamra za
maika 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar,yenye kauli mbiu “Miaka 61 ya
Mapinduzi :Amani ,Umoja na Mshikamano kwa Maendeleo yetu.
Makamu wa Pili wa Rais Mstaafu Balozi Seif Ali Idi akitoa hotuba katika
hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi Mahkama ya Mkoa wa Kusini Bungi
Wilaya ya Kati Unguja.Ikiwa ni Katika Shamra shamra za maika 61 ya
Mapinduzi ya Zanzibar,yenye kauli mbiu “Miaka 61 ya Mapinduzi :Amani
,Umoja na Mshikamano kwa Maendeleo yetu.