MWENYEKITI CCM KIBAHA MJI AWATAKA WENYEVITI WAPYA KUACHA TABIA YA KUJIKWEZA

NA VICTOR MASANGU, KIBAHA

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) Mwalimu Mwajuma Nyamka amewataka wenyeviti wote wa serikali za mitaa kupitia tiketi ya CCM ambao wamechaguliwa kwa kishindo katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika Novemba 27 mwaka huu kutumia madaraka yao vizuri na kufanya kazi kwa weledi na kuwatumikia wananchi kwa kusikiliza kero na chanagmoto zinazowakabili ili kuzitafutia ufumbuzi katika maeneo yao.

Nyamka ameyasema hayo wakati wa halfa fupi ya kuwapongeza wenyeviti wa serikali za mitaa iliyofanyika katika mtaa wa Vikawe Shule kupitia tiketi ya CCM waliopo katika kata ya Pangani Halmasahuri Kibaha mjini ambao wameweza kuibuka ushindi wa kishindo na kufanikiwa kuichukua mitaa yote nane iliyopo ndani ya kata ya Pangani.

Nyamka alisema kwamba kwa sasa wenyeviti wa serikali za mitaa ambao wamechaguliwa wanapaswa kutambua kwamba wamechaguliwa kupitia tiketi ya cahama cha mapinduzi (CCM) hivyo wanawajibu mkubwa wa kuhakikisha kwamba wanatekeleza majukumu yao ipasavyo kwa kutekeleza ilani ya chama ikiwa pamoja na kuwatumikia wananchi kwa kuwaletea kasi ya maendeleo na sio vinginevyo.

Aidha Nyamka aliwapongeza kwa dhati wenyeviti wote kutoka mitaa yote nane iliyopo katika Kata ya Pangani na kuwahimiza kwa sasa wanatakiwa kuungana kwa pamoja na kuweza kujiandaa na uchaguzi mkuu wa mwaka huu wa 2025 ili wagombea wa CCM katika nafasi za Udiwani, Ubunge, pamoja na Urais waweze kushinda kwa kishindo.

“Ndugu zangu tumemaliza uchaguzi wa serikali za mitaa lakini kitu kikubwa ninawaomba wenyeviti wote katika mitaa yote 73 ya Kibaha mji ambao wamechaguliwa kwa kishindo ni kujipanga sasa na kuelekeza nguvu zao zote katika uchaguzi mwingine na kupambana kwa hali na mali kama wao walivyopambaniwa mpaka wakaweza kushinda,”aliongeza Nyamka.

Kwa upande wake Mwenyekiti mpya wa serikali ya mtaa wa Vikawe shule Shaban Shaban amewashukuru kwa dhati wanachama wote wa ccm,viongozi pamoja na wananchi kwa ujumla kwa kuweza kumchagua kuwa kiongozi wao pamoja na kuweza kuwatumikia katika mambo mbali mbali ya kimaendeleo.

Mwenyekiti huyo ameongeza kuwa ameahidi kuitumia nafasi hiyo ambayo amepatiwa kwa kuweza kuhakikisha kwamba anaweka mikakati madhubuti ya kuweza kushirikiana bega bega na wananchi pamoja na Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini kwa ajili ya kuweza kuleta chacu ya maendeleo katika nyanja mbali mbali.

“Kwa kweli nipende kuchukua fursa hii ya kipekee kwa wanachama wote wa CCM,kwa kuweza kunipa kuranyingi ambazo zimeweza kupelekea ni mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Vikawe shule na mimi kwa nafasi yangu nitakuwa mstari wa mbele katika kusikiliza changamoto mbali mbali ambzo zinawakabili wananchi ili ziweze kufanyiwa kazi,”alisema Mwenyekiti Shabani.

Naye Diwani wa Kata ya Pangani Agustino Mdachi alisema kwamba atahakikisha anashirikiana na wenyeviti wote ambao wameweza kushinda ili waweze kusikiliza changamoto mbali mbali za wananchi zinazowakabili katika nyanja za afya, elimu,maji pamoja na mambo mengine ya msingi na kuzitafutia ufumbuzi.


Nao baadhi ya viongozi wa CCM mtaa wa Vikawe shule wamepongeza kwa dhati Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kibaha mjini Mwalimu Mwajuma Nyamka pamoja na Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka kwa kuweza kuwa mstari wa mbele kutekeleza Ilani ya Chama kwa vitendo ikiwa sambamba na kuwaletea maendeleo wananchi katika nyanja mbali mbali.


 

Related Posts