Kifungo cha usajili chaiamsha Mtibwa

BAADA ya FIFA kuifungia Mtibwa Sugar kusajili kutokana na kutomlipa kipa Justin Ndikumana aliyekuwa akiidakia timu hiyo.

msemaji wa klabu hiyo Thobias Kifaru, amesema watakaa na mwanasheria wajue wanafanya kitu gani.

Kifaru alikiri kuwapo kwa adhabu hiyo, lakini hadi wakae na mwanasheria ndipo watajua kipi watakizungumza na vyombo vya habari.

“Nikiri tumeona adhabu hiyo, ila sitaweza kuzungumza chochote hadi tukae na mwanasheria tujue kipi tutakifanya,” alisema.

Kabla ya FIFA kutoa  adhabu hiyo, Mtibwa ilitakiwa kumlipa Ndikumana mshahara wa miezi 11 ya mkataba uliokuwa umebakia na adhabu nyingine za miezi mitatu na ilipewa siku 45 ambazo mwisho ilikuwa ni Januari 2.

Alipotafutwa  Ndikumana, raia wa Burundi kuhusiana na ishu hiyo alisema: “Kila kitu kimekaa kisheria, lengo asiwepo mtu ambaye ataonewa ama kudhulumiwa haki yake kama ilivyoagiza FIFA ndio maana inakuwa ngumu mimi kusema chochote kwa sasa.”

Kipa huyo ambaye aliwahi kuichezea Coastal Union ya Tanga, hakuweza kuendelea kuitumikia Mtibwa baada ya timu hiyo ya Manungu kushuka daraja.

Ndikumana licha ya kutotaka kuzungumzia atajiunga na timu gani, Mwanaspoti linafahamu anazungumza na Sofapaka ya Kenya aliyowahi kuichezea miaka ya nyuma.

Related Posts