WAZIRI KOMBO AAGANA NA BALOZI WA ALGERIA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo amekutana na Balozi wa Algeria nchini Mhe. Ahmed Djellal aliyefika katika ofisi za Wizara Dar es Salaam kutoa shukrani na kuaga akiwa anaelekea ukingoni mwa kuhudumia nchini Tanzania.

Kwa pamoja viongozi hao wawili wamekumbushana kuhusu historia nzuri ya uwili kati ya Tanzania na Algeria iliyoanza kabla ya Uhuru na kuendelea kunawiri hadi sasa.

Waziri Kombo ameishukuru Algeria kwa ushirikiano mzuri wa kimaendeleo na kuahidi kukuza ushirikiano wa kibiashara baina ya Tanzania na Algeria.

Kwa upande wake Balozi Djellal ameshukuru kwa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano iliyofanyika mwaka 2023. Aidha, ameipongeza Wizara kwa kuanzisha Jarida la ‘Foreign Affairs Bulletin’ ambalo limetoka kwa mara ya kwanza mwezi Oktoba.








Related Posts