Riadha Kilimanjaro yapata mabosi wapya

CHAMA cha Riadha Mkoa wa Kilimanjaro kimepata mabosi wapya baada ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa chama hicho uliofanyika leo katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, huku Mwenyekiti wa zamani Adram Mikumi akiangushwa na Nelson Mrashani.

Katika uchaguzi huo Mrashani alipata kura 17 na kumshinda Mikumi aliyepata sita, ilhali nafasi ya Makamu Mwenyekiti ikichukuliwa na Gilbert Semgonja aliyekuwa hana mpinzani.

Katika uchaguzi huo, Katibu Mkuu ilichukuliwa na Michael Luhanjo aliyetetea nafasi bila ya kupingwa, wakati nafasi ya Mhazini ikichukuliwa na Batuli Msangi ambaye kama ilivyokuwa kwa Makamu Mwenyekiti na Katibu Mkuu alipita bila yua kupingwa.

Mwenyekiti mpya katika uongozi wake atajitahidi kukuza mapato kwenye chama hicho cha riadha,kwani Mkoa wa Kilimanjaro ni miongoni inayoongoza kuwa na mbio nyingi zinazoazishwa wilayani, atajitahidi kusaka vipaji kupitia mashuleni, kuanda riadha kwa kila wilaya ilikupata wanariadhaa bora wa kimataifa.

Related Posts