NAIBU WAZIRI KUNDO AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA VISIMA VYA MAJI VIJIJI VITANO RUANGWA

Naibu waziri wa maji Mhandisi Kundo Andrea Methew ameweka jiwe la msingi katika mradi wa uchimbaji visima na ujenzi miundombinu rahisi wa shilingi milioni 325 katika vijiji vitano wilayani Ruangwa Mkoani Lindi.

Mradi huo wa uchimbaji wa visima na ujenzi wa miundombinu rahisi katika vijiji vitano ambavyo havina huduma ya maji ni program maalum ya Serikali ya uchimbaji visima 900 inatekelezwa Nchi mzima katika Majimbo yote ya uchaguzi.

Akizungumza mara baada ya kukagua na kuweka jiwe la msingi katika kisima cha maji huko katika kijiji cha Mmawa Mhandisi kundo ametoa maelekezo kwa wakala wa maji na usafi wa mazingira kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati.

Amesema mpaka kufikia tarehe 31 mwezi huu maeneo yote ambayo hayajakamilika kutoa huduma yaanze kutoa huduma kama dhamamira ya Serikali ilivyotarajia .

Pia ameeleza kuwa Serikali ya Rais Samia inaendelea kutoa fedha za kutosha kwa ajili ya utekelezaji wa mradi ya maji lengo ni kuhakikisha wanqnchi wote wanapata huduma hiyo kwa ukaribu zaidi.

Hata hivyo alimtaka mhadisi wa maji kuhakikisha anafanya maboresho katika baadhi ya maeneo ikiwa pamoja na mita na presha ya utokaji wa maji kwenye mabomba.

Kwa upande wake meneja wa Ruwasa wilaya ya Ruangwa Lawrence Mapunda amesema mradi huo unatekelezwa kwa kutumia force akaunt ambapo ujenzi wa miundombinu kwa sasa mradi huo umefikia asilimia 85% .

Mradi huo utakapokamilika utawanufa jumla ya kaya 917 kutoka katika vijiji vitano ambavyo ni Mmawa , Mtawilile , Njawale, Mpara na Namkatila huku ikiongeza hali ya upatikanaji wa huduma ya maji vijijini kwa asilimia 2.62 kutoka asilimia 74.8 hadi kufikia asilimia 77.42.

Amesema miradi hiyo itakapokamilika itaendeshaa na kusimamiwa na wananchi wenyewe kupitia vyombo vya watumia maji.

 

Related Posts