Serikali kuunda kamati maalum kushughulikia hoja za CAG kila mwaka -DK.Mwinyi

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itafanyia kazi changamoto zote zilizojitokeza katika ripoti ya CAG na kuunda kamati maalum itakayoshughulikia kasoro za kiutendaji zinazotokana na hoja za CAG kila mwaka.

Amemtaka Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Mhandisi Zena Ahmed Said kuunda kamati hiyo.

 

Rais Dk.Mwinyi amesema hayo baada Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar , Dk.Othman Abbas Ali kuwasilisha ripoti yake ya ukaguzi kwa mwaka 2022/23 iliyofanyika viwanja vya Ikulu Zanzibar tarehe: 13 Mei 2024.

Aidha Rais Dk.Mwinyi ameendelea kusisitiza kuheshimiwa Ofisi ya CAG na kutoingilia kwa mujibu wa katiba katika kutimiza majukumu yake kwa uhuru.

Rais Dk.Mwinyi ameeleza kuwa ameridhika kwa hatua za mafanikio ya zaidi ya asilimia 90 ya hati za ukaguzi zinazoridhisha katika ripoti ya mwaka 2022/23.

Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi amebainisha kuwa Serikali ikijikita kujiendesha kwa njia ya mifumo ya kidijitali katika kila nyanja itasaidia kupiga hatua za maendeleo kwa haraka.

Related Posts