Straika Mtanzania arejea Bongo | Mwanaspoti

STRAIKA wa zamani wa Fleetwoods United FC, Mgaya Ally iliyokuwa inashiriki Ligi Darala la Pili UAE yuko Bongo akiwindwa na Coastal Union ya Tanga.

Nyota huyo alimaliza mkataba wa miaka miwili hivi karibuni na kabla ya kucheza Falme za Kiarabu aliwahi kutumikia Coastal Union ya vijana U-20 msimu wa 2020/21.

Hapo awali Mgaya alihusishwa na Kagera Sugar ambao tayari walishazungumza lakini dili liligeuka baada ya kocha Melis Medo kumuhitaji Moubarack Amza ambaye tayari imemtambulisha.

Mmoja wa watu wa karibu wa straika huyo aliliambia Mwanaspoti kuwa kuna uwezekano mkubwa wa Mgaya kumalizana na Coastal ambayo imeonyesha nia ya kumsajili.

“Unajua pale Coastal wamemlea na kumkuza hadi kwenda nje, walimruhusu aondoke na sasa mazungumzo yamefikia pazuri na huenda ndani ya wiki hii akasaini mkataba wa miaka miwili,” alisema mtu huyo.

Mbali na dili la Coastal straika huyo alikuwa na ofa kutoka nchi nne yaani Oman, Kazakhstan, Jordan na Hispania ambako zilishindwa kukamilika.

Related Posts