Mradi wa maji kunufaisha zaidi ya watu elfu 7

Zaidi ya wananchi elfu 7 kutoka katika vitongoji vitatu kwenye kata ya Mlafu katika Halmashauri ya wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa wanatarajia kuanza kupata maji safi na salama baada ya Serikali kutenga Shilingi Bilioni Moja kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa maji na hivyo kumaliza kero ya kukosekana maji kwenye maeneo hayo ambayo imedumu kwa miaka zaidi ya 60 toka wakati wa Uhuru.

Licha uwepo wa baadhi ya changamoto za maji ktk baadhi ya maeneo, Serikali imeendelea kuzitatua kwa kadri uwezo wa kibajeti ambapo katika Kata ya Mlafu wilayani Kilolo ni moja ya meneo yaliyokosa maji kwa miaka nenda rudi.

Ayo Tv imezungumza na Diwani wa kata ya Mlafu Isdori Kiengi na amesema ” tangu uhuru kata hiyi haijawai pata maji ya Bomba kama ilivyo kwa wengine Hadi Kuna wakati tulikuwa tunafikiri sisi sio watanzania lakini tunaishukuru serikali yetu imetusikia na Sasa mradi wa maji utaanza kutekelezwa katika Kijiji chetu ” Amesema Diwani wa kata ya Mlafu.

Hatahivyo meneja wa maji Iringa katika mji mdogo wa Ilula Aron Mussa amesema mradi huo wa maji utatekelezwa kwa siku 365 yaani Mwaka mmoja na tiari mkandarasi ameshatia saini mkataba na mradi huo unagharimu bilioni Moja

Related Posts