Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amesema chama hicho ni kikubwa kuliko mtu yeyote na kuwataka wanachama wote kukilinda kwa nguvu zao zote.
Mbowe ameyasema hayo leo wakati akihutubia kwenye Baraza la Wazee wa Chadema (Bazecha) lililokutana leo kwa ajili ya uchaguzi wa viongozi wao.