Madai ya rushwa uchaguzi Bavicha, wenyewe wafafanua

Dar es Salaam. Sintofahamu imezuka katika uchaguzi wa viongozi wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) ngazi ya Taifa, baada ya wajumbe kumtilia shaka mmoja wa wagombea aliyekuwa akitoa nauli.

Uchaguzi wa Bavicha unaendelea katika ukumbi wa Ubungo Plaza, jijini Dar es Salaam usiku huu Jumanne Januari 14, 2025.

Mashaka zaidi yametokana na mgombea huyo kudaiwa kugawa nauli hizo katika eneo la kificho, wajumbe wakiuliza ana mamlaka gani ya kutoa fedha hizo.

Hali hiyo ilizua tafrani baada ya wajumbe kutoka ukumbini kwenda alikokuwa mgombea huyo, wakihoji yeye ni nani hadi atoe nauli kwa wajumbe.

Hata hivyo, muda mchache baada ya video hiyo kusambaa, Bavicha kupitia ukurasa wake wa X (zamani Twitter) limefafanua huku likisema haikuwa rushwa.

“Si kweli kuwa kuna mazingira ya rushwa. Idrissa Kassim alikabidhiwa fedha za nauli kwa wajumbe wa Bavicha kutoka Kanda ya Magharibi, wakati akiwalipa ndio ilitafsiriwa kuwa anatoa rushwa,”imeandika Bavicha.

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi

Related Posts