MEJA JENERALI MABELE AFUNGA MAFUNZO YA AWALI YA KIJESHI RWAMKOMA 822 KJ

 

MKUU wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Rajabu Mabele,akikagua gwaride la heshima  la Vijana wa mafunzo ya JKT wakati wa hafla ya kuhitimisha zoezi la ufungaji  mafunzo ya awali ya Kijeshi kwa Vijana wa kujitolea Operesheni miaka 60 ya JKT katika Kikosi cha Jeshi 822 KJ Rwamkoma wilayani Butiama Mkoani Mara.

Na.Alex Sonna-BUTIAMA

MKUU wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Rajabu Mabele,ameipongeza Serikali kwa kuendelea kuwekeza kwenye mafunzo ya vijana hali inayofanya Tanzania kuendelea kuwa salama wakati wote.

Meja Jenerali Mabele ameyasema hayo leo Mei 13,2024 wakati wa hafla ya kuhitimisha zoezi la ufungaji  mafunzo ya awali ya Kijeshi kwa Vijana wa kujitolea Operesheni miaka 60 ya JKT katika Kikosi cha Jeshi 822 KJ Rwamkoma wilayani Butiama Mkoani Mara.

Amesema kuwa Serikali inatambua na kuthamini umuhimu wa mafunzo ya JKT ndio maana imeendelea kuiongezea JKT uwezo ili vijana wengi wapate nafasi ya kujiunga katika mafunzo ya JKT.

“Serikali imekuwa ikiboresha miundombinu ya Makambi na Vikosi vya JKT ili kuliwezesha kuchukua vijana wengi kwa ajili ya kupatiwa mafunzo hayo”. amesema Meja Jenerali Mabele.

Aidha amewataka kuhakikisha wanalinda Taifa,wanasimamia miongozo,uadilifu na maelekezo ya kila siku ili nchi iendelee kuwa salama.

Katika hatua nyingine Meja Jenerali Mabele,amezindua  rasmi mitandao ya kijamii ya JKT ambayo ni Twitter, Instagram na Facebook ili kuupa wigo umma wa watanzania kupata habari mbalimbali zinazohusu JKT.

“Kwakuwa dunia kwa Sasa ipo kiganjani hivyo nasi JKT tunalitambulisha jukwaa la mitandao ya kijamii kuwa moja ya eneo ambalo jamii itaweza kupata habari zetu kwa uhakika mbali na ile njia ya tovuti, hususani katika kipindi cha kutangaza nafasi za kujiunga na mafunzo ya Mujibu wa Sheria na Kujitolea”.ameongeza Meja Jenerali Mabele.

Kwa upande wake Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob Mkunda, Mkurugenzi wa Utumishi kutoka Tawi la Utumishi Jeshini Brigedia Jenerali Simon Pigapiga amewataka wahitimu hao kuwa mabalozi wazuri na kujiepusha na vitendo viovu.

“Niwasihi mkawe vijana bora wakati wote kwa kujiepusha na vitendo viovu vitakavyowasababishia matatizo ya afya ya mwili na akili”. amesema Brigedia Jenerali Pigapiga.

Naye Mkuu wa Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) Kanali Makame Daima amesema kuwa JKU inaendelea kujifunza kutoka kwa JKT kutokana na ushirirkiano uliopo baina ya vyombo hivyo viwili.

“Nimekuwa nikipokea maelekezo toka kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa kuitaka JKU kuwa kama JKT, nami natekeleza agizo hilo kwa vitendo”.amesisitiza  Kanali Daima.

Akitoa taarifa ya mafunzo ya Kujitolea Operesheni Miaka 60 ya JKT, Mkuu wa Tawi la Mafunzo na Operesheni JKT Kanali Aisha Matanza amesema mafunzo hayo yamechukua jumla ya majuma 16 mfululizo.

“Vijana hawa wanawawakilisha vijana wenzao ambao wamefanya mafunzo kama haya katika vikosi vingine vya JKT”. amesema Kanali Matanza.

Awali  Kamanda Kikosi Luteni Kanali Gaudencia Mapunda,amesema kuwa mafunzo waliyoyapata vijana hao yamewajengea Uzalendo, Uadilifu na uwajibikaji kwa Taifa lao.

” Hadi kufikia hii leo wahitimu hawa wamefikia malengo yao ya mafunzo haya kwa kiwango cha juu”. amesema Kanali Mapunda.

Mafunzo ya awali ya kijeshi kwa vijana wa Kujitolea Operesheni Miaka 60 ya JKT yamefungwa katika vikosi 19 vya Jeshi la Kujenga Taifa ambapo baada ya mafunzo hayo vijana hao wanaenda kuanza hatua nyingine ya mafunzo ya stadi za maisha na stadi za kazi katika vikosi mbalimbali kwa muda wa miezi 20 ili kukamilisha miaka miwili ya mkataba wao na JKT.

MKUU wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Rajabu Mabele,akikagua gwaride la heshima  la Vijana wa mafunzo ya JKT wakati wa hafla ya kuhitimisha zoezi la ufungaji  mafunzo ya awali ya Kijeshi kwa Vijana wa kujitolea Operesheni miaka 60 ya JKT katika Kikosi cha Jeshi 822 KJ Rwamkoma wilayani Butiama Mkoani Mara.

MKUU wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Rajabu Mabele,akishuhudia kiapo cha utii kutoka kwa vijana wa  mafunzo ya JKT wakati wa hafla ya kuhitimisha zoezi la ufungaji  mafunzo ya awali ya Kijeshi kwa Vijana wa kujitolea Operesheni miaka 60 ya JKT katika Kikosi cha Jeshi 822 KJ Rwamkoma wilayani Butiama Mkoani Mara.

Gwaride la Heshima la Vijana wa kujitolea likipita mbele ya mgeni rasmi Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Rajabu Mabele,(hayupo pichani)  wakati wa hafla ya kuhitimisha zoezi la ufungaji  mafunzo ya awali ya Kijeshi kwa Vijana wa kujitolea Operesheni miaka 60 ya JKT katika Kikosi cha Jeshi 822 KJ Rwamkoma wilayani Butiama Mkoani Mara.

MKUU wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Rajabu Mabele, akizungumza wakati wa hafla ya kuhitimisha zoezi la ufungaji  mafunzo ya awali ya Kijeshi kwa Vijana wa kujitolea Operesheni miaka 60 ya JKT katika Kikosi cha Jeshi 822 KJ Rwamkoma wilayani Butiama Mkoani Mara.

MKUU wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Rajabu Mabele,akizindua  mitandao ya kijamii ya JKT ambayo ni Twitter, Instagram na Facebook ili kuupa wigo umma wa watanzania kupata habari mbalimbali zinazohusu JKT wakati wa hafla ya kuhitimisha zoezi la ufungaji  mafunzo ya awali ya Kijeshi kwa Vijana wa kujitolea Operesheni miaka 60 ya JKT katika Kikosi cha Jeshi 822 KJ Rwamkoma wilayani Butiama Mkoani Mara.

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob Mkunda, Mkurugenzi wa Utumishi kutoka Tawi la Utumishi Jeshini Brigedia Jenerali Simon Pigapiga,akizungumza wakati wa hafla ya kuhitimisha zoezi la ufungaji  mafunzo ya awali ya Kijeshi kwa Vijana wa kujitolea Operesheni miaka 60 ya JKT katika Kikosi cha Jeshi 822 KJ Rwamkoma wilayani Butiama Mkoani Mara.

Mkuu wa Tawi la Mafunzo na Operesheni JKT Kanali Aisha Matanza, akizungumza  wakati wa hafla ya kuhitimisha zoezi la ufungaji  mafunzo ya awali ya Kijeshi kwa Vijana wa kujitolea Operesheni miaka 60 ya JKT katika Kikosi cha Jeshi 822 KJ Rwamkoma wilayani Butiama Mkoani Mara.

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) Kanali Makame Daima,akizungumza  wakati wa hafla ya kuhitimisha zoezi la ufungaji  mafunzo ya awali ya Kijeshi kwa Vijana wa kujitolea Operesheni miaka 60 ya JKT katika Kikosi cha Jeshi 822 KJ Rwamkoma wilayani Butiama Mkoani Mara.

Kamanda Kikosi Luteni Kanali Gaudencia Mapunda,akizungumza  wakati wa hafla ya kuhitimisha zoezi la ufungaji  mafunzo ya awali ya Kijeshi kwa Vijana wa kujitolea Operesheni miaka 60 ya JKT katika Kikosi cha Jeshi 822 KJ Rwamkoma wilayani Butiama Mkoani Mara.

MKUU wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Rajabu Mabele, akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuhitimisha zoezi la ufungaji  mafunzo ya awali ya Kijeshi kwa Vijana wa kujitolea Operesheni miaka 60 ya JKT katika Kikosi cha Jeshi 822 KJ Rwamkoma wilayani Butiama Mkoani Mara.

Related Posts