Mkuu wa Wilaya Mbozi afariki dunia

Mbeya. Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Ester Mahawe amefariki dunia.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa), Mohamed Mchengerwa kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza kifo cha mkuu huyo wa wilaya kilichotokea leo Januari 14, 2025 katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini (KCMC) mkoani Kilimanjaro alikokuwa akipatiwa matibabu.

Katika taarifa iliyotolewa na Nteghenjwa Hosseah, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Ofisi ya Rais (Tamisemi), Mchengerwa ametoa pole kwa familia, mkuu wa Mkoa wa Songwe, wafanyakazi na wananchi wote wa Wilaya ya Mbozi, ndugu, jamaa na marafiki.

“Ofisi ya Rais Tamisemi kwa kushirikiana na familia inaendelea kuratibu shughuli za mazishi na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa,” inaeleza taarifa hiyo.

Endelea kufuatilia Mwananchi.

Related Posts