Mwandishi Wetu
Daktari Bingwa wa Magongwa yasioambukizwa, Pro. Kaushik Ramary, amepata Tuzo ya Kimataifa, kwa kutambua mchango wake katika kuwasaidia jamii inayosumbuliwa na magonjwa yasioambukizwa na magonjwa mengine inchini Tanzania.
“Kwa kweli tunajivunia sana Tuzo hii aliyopata Pro. Kaushik, Hii inathibitishi kujitoa kwake katika kuwasaidia jamii inayosumbaliw na matatizo mbalimbali ya afya,” kwa mujibu ya taarifa iliyotolewa na Bodi ya Wakurugenzi ya Umoja wa Vituo vya Afya Binafsi nchini Tanzania (APHFTA)
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mapokezi ya Pro. Kaushik, jijini Dar es Salaam, Makamu Raisi wa APHFTA Bw. Mahmoud Mringo amesema “Taasisi inampongeza Profesa Kaushik Ramaiya kwa Kupokea Tuzo ya Kifahari ya Pravasi Bharatiya Samman 2025.”
Tuzo hii heshima ya utambuzi wa juu kabisa unaotolewa na Serikali wa India kwa Wahindi waishio ng’ambo kwa kutambua michango yao adhimu katika nyanja zao na jukumu lao katika kuimarisha mahusiano kati ya India na jumuiya ya kimataifa.
Profesa Kaushik alipokea tuzo hii adhimu kutoka kwa Mhe, Rais wa India, wakati wa Mkutano wa Pravasi Bharatiya Divas huko Bhubaneswar, Odisha, India. Utambuzi huu unasherehekea mafanikio makubwa ya Profesa Kaushik katika huduma za afya, mchango wake muhimu katika kuboresha afya ya umma, na juhudi zake zisizo na kikomo katika kukuza ushirikiano wa kimataifa.
“Kama mwanachama muhimu wa jumuiya ya kimataifa ya huduma za afya, Profesa Kaushik ameonyesha dhamira isiyo na kifani katika kuboresha mifumo ya afya, si tu nchini Tanzania, bali pia katika sehemu mbalimbali duniani.
“Maono yake ya ubunifu, kujitolea kwa ubora wa kitaaluma, na huduma yake yenye huruma imeleta matokeo chanya kwa maisha ya watu wengi na kuwahamasisha kutoa huduma ubora,,” amesem Mringo.
Ameongeza wao kama APHFTA, wanajivunia kuhusishwa na mtu mashuhuri ambaye kazi yake inaendana na dhamira yao ya kuboresha huduma za afya nchini Tanzania.
Amesema mafanikio na utambuzi wa Profesa Kaushik ni uthibitisho wa uwezo wa ushirikiano wa kuvuka mpaka na umuhimu wa ubunifu katika kuleta mabadiliko chanya katika huduma za afya.
Kwa upande wake, Meneja Mipango wa Taasisi ya Magonjwa ya Kisukari nchini (TDA), Dk.Rachael Nungu, amesema “tunatoa pongezi zetu za dhati kwa Profesa Kaushik Ramaiya na shukurani zetu kwa mchango wake muhimu kwa jamii. Kutambuliwa kwake kimataifa ni wakati wa kuona fahari si tu kwa TDA na APHFTA, lakini pia kwa wale wote wanaojitolea kuendeleza huduma za afya duniani kote.”
Wakati huo huo Pro. Kaushik, ambae amefanya kazi kwa Miaka zaidi ya 40 kushughulikia magonjwa yasioambukizwa, amewataka madaktari na wataalam mbalimbali kufanya kazi kwa bidii na kujitolea kikamilifu katika kuwasaidia wahitaji, kwani juhudi na kujitoa kwao katika kuwasaidia watu wenye matatizo kutalipw Mungu.’
Katika taarifa yake, Wizara ya Afya, imesema “Tuzo hii yenye hadhi ya juu na kimataifa inatokana na mchango wake (Pro. Kaushik) wa dhati na Mkubwa anaotoa katika sekta ya Afya nchini Tanzania.”