Dar es Salaam. Kada wa Chadema, Deogratius Mahinyila ameshinda nafasi ya uenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) Taifa, dhidi ya mpinzani wake, Masoud Mambo.
Katika uchaguzi huo, ulioanza jana na kutamatika leo, Januari 14, 2025, Mahinyila ameshinda kwa kupata kura 204 dhidi ya kura 112 alizopata Mambo.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Uchaguzi huo, Elisha Chonya mkutano huo ulikuwa na jumla ya wapiga kura 317, kati yao mmoja kura yake iliharibika, huku 316 zikiwa halali.
Sambamba na Mahinyila, Necto Kitiga ameongoza kura za nafasi ya makamu mwenyekiti bara wa baraza hilo, akiwapiku wenzake wanne.
Necto ameongoza kwa kupata kura 101, akichuana karibu na Juma Ng’itu aliyepata kura 90.
Hata hivyo, kuongoza huko hakukumwezesha Necto kushinda nafasi hiyo kwa kuwa hakufikisha zaidi ya asilimia 50 ya kura, hivyo uchaguzi wa nafasi hiyo utarudiwa.
Endelea kufuatilia Mwananchi.