*Wafurahia meli kutumia siku tatu bandarini, gharama zapungua,wenye mizigo nao wapewa neno
Na Said Mwishehe,Michuzi TV
MABORESHO ambayo yamefanywa katika Bandari ya Dar es Salaam hasa katika upande wa kupakia na kupakua makontena ya mzigo katika meli umesababisha kupungua kwa siku za wafanyabiashara kupokea kontena baada ya meli kutia nanga kutoka siku 10 hadi kufikia siku tatu.
Hayo yameelezwa leo jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Abeid Galusi wakati wa ziara iliyofanywa na Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania ambao wamefika katika bandari hiyo kuona shughuli zinavyoendelea sambamba na kuipongeza Serikali kwa kufanya maboresha yenye tija kubwa.
Amefafanua kuwa mabadiliko hayo yametokana na uwekezaji uliofanywa na kampuni ya DP World pamoja na ADNA ambapo kwa sasa hakuna tena msongamano wa meli kwani zinatumia siku chache na changamoto iliyopo sasa mizigo inarundikana bandari kwasababu wafanyabiashara wanashindwa kutoa mizigo kwa wakati.
“Tunaomba wateja wetu waje kuchukua mizigo kwa wakati kwasababu hivi sasa kuna mizigo mingi haijachukuliwa licha ya kuwa imeshushwa katika meli.Kutokana na maboresho ambayo yamefanyika wateja wetu kasi yamizigo ipo mingi hivyo waongeze kasi ya kuchukua mizigo imekuwa ndogo ukilinganisha na kasi ya kushusha,”amesisitiza Galusi.
Ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa uingizaji wa mizigo katika bandari hiyo umeongezeka kwa asilimia 60 kwa nchi jirani wakati mizogo ya ndani kuna ongezeko la asilimia 40.
Kwa upande wake Meneja wa Uhusiano wa DP World Elitunu Mallamia amesema kwamba wamejitahidi kuongeza ufanisi na kuvunja rekodi Kwa Desemba wamehudumia meli 27 na changamoto iliyopo sasa wateja kushindwa kuondosha mizigo bandarini.
Amesema wanatoa rai kwa wateja kuondosha mizigo yao mapema ili nao waongeze kasi ya kushusha makontena katika ICD huku akiongeza kontena zaidi 220000 zimeingia na kama bandari wamevuka malengo.
Awali Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Tanzania( JWT), Hamis Livembe amesema ufanisi wa ushushwaji wa mizigo bandarini kwa wakati unaimarisha biashara na kuongeza wateja kutoka nje ya nchi ambao wataamua kutumia bandari ya Tanzania na kuachana na nchi nyingine
Alisema lengo la kutembelea bandari ya Dar es Salaam ni kujionea shughuli za upakiaji na ushushwaji wa mzigo na kufafanua kwa sasa kushusha mzigo bandarini ni siku tatu tu ikiwa tofauti na huko nyuma.
“Zamani tulikuwa tunaagiza mzigo lakini tunachukua siku 40 ndio uwe umepata mzigo lakini siku hizi unaweza kuagiza mzigo na ndani ya siku 10 unaupata, hivyo kwa mwezi mfanyabiashara anaweza kuagiza mzigo mara lakini maboresho haya yametusaidia kupunguza gharama sana.”
Ameongeza ucheweleshaji wa meli kuingia bandarini ulisababisha meli kupqnga foleni katika ufukwe wa bahari ya Hindi eneo la Coco Beach ambapo zinakaa maeneo hayo kwa siku 30 mpaka 40 lakini ujio wa DP World umemaliza changamoto hiyo.