Airtel Tanzania imeendesha droo ya nne ya Airtel Santa Mizawadi, ambayo inahitimisha kampeni hiyo maalum iliyolenga kubadilisha Maisha ya wateja na mawakala wa mtandao huo wa simu za mkononi.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam leo Januari 14, 2024, Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano, Jackson Mmbando amesema lengo la zawadi hizo ni kuwasaidia watu kuanza mwaka vizuri katika kushiriki shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii mwanzoni mwa mwaka 2025.
Pia mshindi wa droo ya kwanza ya Airtel Santa Mizawadi, Bi Fatma Mwandege, mkazi wa Majumba sita jijini Dar es Salaam alikabidhiwa zawadi yake ya Pikipiki mpya aina ya TVS ambapo aliishukuru Airtel kwa zawadi hiyo na kuelezea kuwa itaweza kumsaidia katika Maisha yake ya kila siku.
Meneja masoko na ubunifu wa Airtel, Hussein Simba alieleza kuwa zawadi hizo zimelenga kuboresha Maisha ya wateja wa Airtel katika nyanja mbalimbali ikiwemo kuwainua kiuchumi na kijamii.