MKOA WA PWANI WATAKIWA KUWA NA MIKAKATI MADHUBUTI YA KUKUZA BIASHARA NA KUVUTIA WAWEKEZAJI

Picha ya pamoja Baadhi ya washiriki wakati wa mafunzo ya uendeshaji wa Majadiliano kati ya Sekta ya Umma na Binafsi katika Mkoa wa Pwani, yaliyoratibiwa na Idara ya Uwezeshaji Kiuchumi na Maendeleo ya Sekta Binafsi, kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu.) Tarehe 13 Mei 2024.

MKUU wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Abubakar Kunenge, amelitaka Baraza la Biashara la Mkoa kuja na Mikakati Madhubuti ya Kukuza biashara katika Mkoa huo na kuvutia zaidi wawekezaji katika maeneo mbalimbali, akitolea mfano Sekta ya utalii na viwanda.

Mhe. Kunenge ameyasema hayo leo Tarehe 13 Mei 2024, alipofungua Mafunzo ya uendeshaji wa Majadiliano kati ya Sekta ya Umma na Binafsi katika Mkoa wa Pwani, yaliyoratibiwa na Idara ya Uwezeshaji Kiuchumi na Maendeleo ya Sekta Binafsi, kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu.)

Pamoja na mambo mengine Mhe. Kunenge alimshuruku Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa maono na miongozo yake ya kuliongoza Taifa, Katika muelekeo wa kukuza uchumi kupitia sekta ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Kunenge alisema, Mkoa wa Pwani una wajibu mkubwa wa kutumia fursa hiyo iliyowaleta pamoja kutafakari na kujadili juu ya mafanikio yaliyopatikana na changamoto zilizopo katika mfumo wa majadiliano kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi.

“Mkoa wa Pwani, umejaaliwa kuwa fursa za kipekee za kijiografia na rasilimali nyingi ambazo tukiweza kuzitumia vizuri kupitia mashirikiano ya Sekta Binafsi na Sekta ya Umma tutaweza kupiga hatua kubwa katika maendeleo ya kiuchumi, Inafahamika kwamba kwa muda mrefu Mkoa wa Pwani umekuwa mdau muhimu katika kuchochea ukuaji wa uchumi wa Tanzania kupitia fursa za kijiografia na miundombinu wezeshi ikiwemo barabara, reli, umeme na maji. Fursa hizo zimeufanya Mkoa huu kuwa rahisi kufikika.” Alibanisha Mhe. Kunenge

Aliendelea kusema kuwa, Mafunzo hayo yaende sambamba na majadiliano ya kimkakati ya kukuza ufanisi kwenye viwanda ili kukuza mchango wa Mkoa katika pato la Taifa, na kujadili mambo muhimu kama vile kuwa na eneo maalum la viwanda katika mkoa wa pwani ambapo miundombinu yote muhimu inakuwepo, akitolea mfano Miondombinu ya Barabara na Umeme, “Ni makakati gani ambao tunao kama Baraza la biashara la mkoa ili kuja na mkakati na tujue sisi kama mkoa tunataka kwenda wapi.” Alisisitiza Mhe. Kunenge

Kwa Upande wake, Mkurugenzi wa Idara ya Uwezeshaji Kiuchumi na Maendeleo ya Sekta Binafsi Bw. Conrad Milinga Kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Alisema lengo kubwa la mafunzo haya ni kuwaleta kwa pamoja wadau wa sekta binafsi na sekta ya umma ili kufanya kazi kwa pamoja kwa kutambua pia sekta binafsi ni injini ya uchumi inayoweza kuwekeza, kuongeza Ajira kwa mapana yake na kuchakata na kuongeza thamani ya mazao yanayozalishwa ndani ya nchi ili kuweza kuongeza mapato ya Serikali.

Mafunzo hayo ya siku mbili yenye kaulimbiu inayosema; Imarisha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji wa Uchumi Endelevu, yamehudhuriwa na viongozi wa Mkoa wa Pwani wakiwemo Wakuu wa Wilaya, washiriki kutoka katika sekta Binafsi nchini, Sekta za umma, Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF).

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Abubakar Kunenge akizungumza wakati kikao cha Mafunzo ya uendeshaji wa Majadiliano kati ya Sekta ya Umma na Binafsi katika Mkoa wa Pwani, yaliyoratibiwa na Idara ya Uwezeshaji Kiuchumi na Maendeleo ya Sekta Binafsi, kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu.) Tarehe 13 Mei 2024

Bw. Conrad Milinga , Mkurugenzi wa Idara ya Uwezeshaji Kiuchumi na Maendeleo ya Sekta Binafsi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) akizungumza na Waandishi wa Habari hawapo katika picha wakati wa mafunzo ya uendeshaji wa Majadiliano kati ya Sekta ya Umma na Binafsi katika Mkoa wa Pwani, yaliyoratibiwa na Idara ya Uwezeshaji Kiuchumi na Maendeleo ya Sekta Binafsi, kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu.) Tarehe 13 Mei 2024.

Sehemu ya meza kuu wakati wa mafunzo ya uendeshaji wa Majadiliano kati ya Sekta ya Umma na Binafsi katika Mkoa wa Pwani, yaliyoratibiwa na Idara ya Uwezeshaji Kiuchumi na Maendeleo ya Sekta Binafsi, kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu.) Tarehe 13 Mei 2024

Baadhi ya Washiriki wakati wa mafunzo ya uendeshaji wa Majadiliano kati ya Sekta ya Umma na Binafsi katika Mkoa wa Pwani, yaliyoratibiwa na Idara ya Uwezeshaji Kiuchumi na Maendeleo ya Sekta Binafsi, kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu.) Tarehe 13 Mei 2024

Katikati, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Abubakar Kunenge akizungumza wakati wa kikao cha mafunzo ya uendeshaji wa Majadiliano kati ya Sekta ya Umma na Binafsi katika Mkoa wa Pwani, yaliyoratibiwa na Idara ya Uwezeshaji Kiuchumi na Maendeleo ya Sekta Binafsi, kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu.) Tarehe 13 Mei 2024

Related Posts