Adam, Athuman kufukia mashimo TZ Prisons

KOCHA wa Tanzania Prisons, Amani Josiah amesema mapumziko ya Ligi Kuu Bara yamemsaidia kupata muda wa kuwaangalia wachezaji wanahitaji mazoezi ya aina gani, lakini majembe mapya kikosini yatafukia mashimo.

Kocha huyo aliyetua kikosini akitokea Geita Gold iliyopo Ligi ya Championship, alisema kitu kikubwa alichofanyia kazi ni utimamu wa miili kwa wachezaji pamoja na mambo ya kiufundi anayoamini yatampa matunda katika mzunguko wa pili.

Prisons ipo nafasi ya 13 katika msimamo wa Ligi Kuu ikiwa imecheza mechi 16, imeshinda nne, sare tano, ikipoteza saba ina pointi 17, ikifunga mabao saba na kufungwa 17, jambo ambalo kocha huyo  alisema wana kazi ngumu kuhakikisha wanapambana kupanda nafasi za juu katika msimamo wa ligi.

“Katika kikosi kuna ongezeko la wachezaji wapya kama Adam Adam, Yusuph Athuman, Kelvin Sabato ‘Kiduku’ na wengine ambao wataongeza nguvu na kuziba pengo la wachezaji ambao ni Jeremiah Juma na Samson Mbangula ni majeruhi watakaa nje zaidi ya miezi miwili,” alisema.

Related Posts