KIUNGO wa kimataifa wa Tanzania, Alphonse Mabula aliyekuwa akicheza FK Spartak Subotica ya Serbia, amejiunga na Shamakhi FK inayoshiriki Ligi Kuu Azerbaijan kwa mkataba wa mwaka mmoja na nusu.
Mabula ambaye ana umri wa miaka 21, amesaini mkataba huo baada ya fursa ya usajili kuja wakati wa mapumziko ya majira ya baridi.
Akizungumza kuhusu safari yake ya soka, mchezaji huyo alielezea furaha yake akisema kuwa anahisi kuwa hii ni fursa nyingine ya kuonyesha uwezo wake na kwamba, yupo tayari kukutana na changamoto mpya zinazomkabili katika ligi hiyo.
“Ni fursa nzuri kwangu na najivunia kujiunga na Shamakhi FK. Niko tayari kwa changamoto mpya na ningependa kuleta mchango wangu kwenye timu hii,” alisema.
Mabula anajiunga na Shamakhi FK kutoka FK Spartak Subotica ya Serbia, ambapo alikuwemo kabla ya kuhamia kwa mkopo kwenye klabu ya Novi Sad ya Serbia.
Kwa mujibu wa taarifa inaelezwa kuwamba Mabula ni pendekezo la kocha wa kikosi hicho, Aykhan Abbasov.