Dar es Salaam. Mwanasiasa mkongwe aliyewahi kushika nyadhifa mbalimbali katika Serikali na Chama cha Mapinduzi (CCM), Stephen Wasira ameteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho (Bara).
Wasira ambaye jina lake limewasilishwa mbele ya mkutano mkuu wa CCM unaoendelea jijini Dodoma leo Januari 18, 2025, limepata baraka za Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya chama hicho kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Abdulrahman Kinana aliyetangaza kupumzika miezi mitano iliyopita.
Kwa sasa jina la Wasira litapigiwa kura na wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM.
Endelea kufuatilia Mwananchi.