Zanzibar yatangaza bei mpya ya umeme

Unguja. Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (Zura), imetangaza bei mpya elekezi kwa watumiaji wote wa umeme kisiwani humo ambapo zitaaza rasmi Januari 20, mwaka huu.

Kwa mujibu wa Zura, ilipokea maombi ya kubadilisha bei za umeme kutoka Shirika la Umeme Zanzibar (Zeco) kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya matumizi ya umeme Zanzibar.

Taarifa iliyotolewa na Zura leo Januari 18, 2025, bei hizo zimetoa punguzo la Sh190 kwa watumiaji wadogo ambao walikuwa wakilipa Sh480 kwa uniti kila wanapovuka matumizi ya uniti 50 kwa mwezi ambapo kwa sasa watalipa Sh290 badala ya Sh480.

Meneja wa kitengo cha Uhusiano Zura, Mbaraka Haji amesema tozo ya kutoza huduma kwa watumiaji wadogo kuanzia unit 0 hadi 50 itaendelea kuwa Sh2,100 huku bei ya kuungiwa kwa uniti moja ikiongezeka kutoka Sh79 hadi Sh84.

Wateja wenye matumzi ya kawaida wenye matumzi ya uniti moja hadi 1,500 bei ya kuungiwa kwa uniti moja imepanda kutoka Sh266 hadi Sh280 huku kila uniti inayoongezeka ikitoka Sh288 hadi Sh310 na tozo ya kutoa huduma itaendelea kuwa Sh2100.

“Hwa ni wateja wenye matumzi ya kwaida hususani majumbani wenye biashara ndogondogo, maduka mabango waliounganishwa katika msongo wa mdogo wa umeme kwenye njia moja (230) na njia tatu 400v,” amesema.

Kwa wateja waliounganishwa katika msongo mdogo na msongo wa kati wa umeme, bei ya nishati ya uniti moja imeongezeka kutoka hadi Sh217 huku bei ya mahitaji ya juu itabaki bei ya wali Sh16,000 na tozo ya kutoa huduma itaendelea kuwa bei ileile ya Sh10,500.

Kwa mujibu wa mamlaka hiyo, wateja waliounganishwa katika msongo mkubwa wa umeme bei ya uniti itakuwa Sh178 kutoka Sh169, bei ya mahitaji ya juu itaendela kuwa Sh16,000 na bei ya tozo itaendela kuwa bei ilile Sh150,000.

Mbaraka amesema hatua hiyo imefikiwa baada ya kufanya tathmini ya kina ikiwemo kukutana na wadau ili kupata maoni yao.

Related Posts