Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Dkt. Jakaya Kikwete ametaka kuletwa kwa Azimio la Kumpitisha Dkt Samia Suluhu Hassan na Dkt Hussein Mwinyi kuwa wagombea wa Urais Kupitia CCM katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mapema Mwezi Octoba mwaka huu.
Hatua hii imekuja baada ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu kuleta hoja ya kutaka wagombea Urais Kutangazwa katika Mkutano huu Mkuu Maalumu.