Gadiel arejesha majeshi Singida | Mwanaspoti

BAADA ya kuvunja mkataba na Chippa United ya Afrika Kusini, Mtanzania Gadiel Michael ametimkia Singida Black Stars.

Nyota huyo wa zamani wa Simba na Yanga ambaye wakati mwingine amekuwa akitumika kama kiungo Chippa, alijiunga na timu hiyo msimu huu kwa mkataba wa mwaka mmoja akitokea Cape Town Spurs ya nchini humo.

Siku chache zilizopita alisitisha mkataba na Chippa aliojiunga nao msimu huu huku sababu za kuvunja mkataba huo zikiwa hazijulikani.

Chanzo kililiambia Mwanaspoti beki huyo yuko kwenye hatua za mwisho kujiunga na Singida Black Stars.

“Kama atasaini mkataba utakuwa wa miaka mitatu, hayo ni makubaliano ya awali baada ya kuondoka Afrika Kusini,” kilisema chanzo hiko.

Hata hivyo, gazeti hili liliwatafuta viongozi wa Singida juu ya ishu hiyo ya usajili, lakini hawakupokea simu.

Hadi sasa Singida imesajili wachezaji wanne, kipa Amas Obasogie (Nigeria), Eliuter Mpepo (Tanzania), Jonathan Sowah (Ghana) na Serge Pokou kutoka Ivory Coast.

Related Posts