Hasnath Ubamba atamani rekodi Misri

BAADA ya kufika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa wanawake msimu huu, winga wa FC Masar ya Misri, Hasnath Ubamba amesema anatamani kuweka rekodi nyingine ligi kuu.

Masar ilitolewa nusu fainali na AS Far Rabat ya Morocco kwa jumla ya mabao 2-1 ikiambulia medali ya mshindi wa tatu huku mtanzania huyo akicheza michezo yote.

Akizungumza na Mwanaspoti, Ubamba alisema anatamani kuandika historia nyingine akiwa na mabingwa hao watetezi wa Misri.

“Mungu atusaidie mimi na timu yetu kwa upambanaji wetu na matamanio ya kila mchezaji, natumaini tutafika mbali zaidi ya mwaka jana tulipoishia,” alisema Ubamba.

Aliongeza, licha ya kuchukua ubingwa wa ligi msimu uliopita matamanio yake pia ni kuutetea msimu huu.

Related Posts