Rinazon Ministry Ukombozi kwa Wanandoa – Global Publishers



Muasisi wa huduma ya Rinazon Magreth Misericodias Mushi. 

Rinazon Ministry ni huduma ya kiroho ambayo imekuwa na mkombozi mkubwa kwa wanandoa katika kustawisha ndoa zao na kuzitibu ndoa zote zilizo kwenye changamoto za migogoro isiyokwisha.

Hayo yalisemwa na muasisi wa huduma hiyo, Magreth Misericodias Mushi kwenye hafla miaka mitatu  ya huduma hiyo iliyofanyika jana Jumaosi kwenye Ukumbi wa Mbezi White Park uliopo karibu kabisa na Kituo cha Daladala cha Mbezi Tangi Bovu jijini Dar.

Magreth amesema pamoja na huduma hiyo ikiwa imetimiza miaka mitatu sasa itakuwa ikifanyika kwenye ukumbi huo kila Jumanne.

Magreth ametumia nafasi hiyo kuwakaribisha wote wenye changamoto kwenye ndoa zao na mambo mengine yanayohitaji tiba ya kiroho na hata wasio na changamoto na ndoa zao wanakaribishwa kwaajili ya kuziimarisha na kufunguliwa kutoka kwenye vifungo mbalimbali.

Claudia Paul ni mmoja wa mashuhuda wa huduma hiyo ambaye ndoa yake ilishawahi kuingia kwenye mapito makubwa yaliyomfanya akate tamaa lakini baada ya kufuatilia huduma ya Rinazon kupitia kwenye mitandao ya kijamii sasa ndoa yake imekuwa ni sehemu ya amani na furaha.


Related Posts