KIUNGO mpya wa JKT Queens, Elizabeth John amesema anatamani kufanya makubwa akiwa na timu hiyo kutokana na ubora wa timu hiyo.
Kinda huyo alipewa mkono wa kwaheri na Alliance Girls aliyoitumikia kwa misimu miwili tangu alipojiunga nao mwaka 2022.
Akizungumza na Mwanaspoti, John alisema anatamani kufanya makubwa na kuandika historia akiwa na klabu kubwa kama JKT Queens.
Aliongeza, licha ya ubora wa kikosi cha JKT haimzuii kupambania namba kwani kocha wa timu hiyo, Esta Chabruma amekuwa akiwapa nafasi wachezaji wadogo.
“Unaposajiliwa na timu kubwa kama JKT ambayo ni ndoto ya kila mchezaji wa kike, unapaswa kuwa na juhudi, naamini nitafanya vizuri zaidi ya kule Alliance,” alisema kinda huyo.