Fountain Princess yaongeza saba wapya

FOUNTAIN Gate Princess imeongeza wachezaji saba kutoka mataifa mbalimbali dirisha hili dogo, huku pia ikikamilisha taratibu za vibali kwa nyota wake ambao hapo awali ilishindwa kuwatumia.

Akizungumza na Mwanaspoti, Kocha Mkuu wa Fountain Mirambo Camil alisema ripoti yake imefanyiwa kazi ya kuhitaji karibu kila mchezaji kwenye eneo na sasa wako vitani kujiandaa na ligi.

Aliongeza tatizo la vibali lililowaathiri kwa kiasi kikubwa limetatuliwa hivyo sasa kilichobaki ni kuwatumia tu.

“Ndiyo vibali vililipiwa na tumeongeza wachezaji, hatukuanza vizuri ligi, kwa changamoto hiyo sasa kilichobaki ni kupambana kuhakikisha pointi tulizopoteza zinarudi,” alisema Camil.

Wachezaji waliongezwa ni Annociate Eze (Beki), Suzan Zilfa (Kiungo, Burundi), Irine Madalina (Mshambuliaji, Kenya), Lucia Mrema (kiungo), Rehema Ramadhani (mshambuliaji, Tanzania), Winifrida Casto (kiungo) na Asha kadosho (mshambuliaji, Tanzania).

Related Posts