DKT.EMMANUEL NCHIMBI MGOMBEA MWENZA CCM UCHAGUZI MKUU 2025

Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Dodoma

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Taifa na Mgombea urais wa Uchaguzi Mkuu mwaka 2025 kwa tiketi ya Chama hicho Rais Dk.Samia Suluhu Hassan amemtangaza Dk.Emmanuel Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza wake katika uchaguzi mkuu mwaka 2025 baada ya Kamati Kuu kuridhia jina lake.

Akizungumza mbele ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa Chama Cha Mapinduzi, Dk.Samia amesema kuwa kwa kawaida baada ya kupitishwa jina la Mgombea urais basi hatua inayofuata ni kupitishwa jina la mgombea mwenza.

“Waheshimiwa wajumbe kwa kawaida ya Chama Cha Mapunduz tukishamchagua mgombea urais huwa kamati kuu inakaa na ndilo agizo la Halmashauri Kuu ya Taifa Kwenda kuleta la mgombea mwenza. Nilikwenda kunong’ona na Kamati Kuu kutafuta mgombea mwenza…

“Kama mnavyojua Dk.Philip Mpango ndio Makamu wa Rais lakini miezi ya karibuni alikuja kuniona na kuniomba nimpumzishe na anasababu kadhaa lakini sio za mahusiano ya kazi , anasema sasa ana miaka 68 na angependa kuishi zaidi ikiwezekana agonge miaka 90 aliniambia mama yake ameishi miaka 88 kwa hiyo anataka kumpita mama yake, hivyo anaomba kumzika kwa kuniandikia barua.

“Nilivyokwenda kuzungumza na Kamati Kuu nikaieleza hiyo hali na kwa kauli moja tumemekubaliana tumpunzishe lakini nataka niwaambie Dk.Mpango amekuwa msaada mkubwa sana kwangu, nimemtuma na hakuwa analalamika.

“Baada ya kupata barua ya Makamu wa Raisa nilianza kuhangaika nani atafaa , nikaanza kufikiria nani anaweza kutufa basi nikawa na majina kadhaa… leo kama miliona niliwatoa wazee wangu hawa watatu Dk.Shein, Dk.Kikwete na Dk.Karume nikaenda kuwalilia na kuwaambia hali niliyonayo kwani mkutano huu umezua mambo makubwa, lakini Rais mstaafu Kikwete amenisaidia sana

“Jina moja ndlo ambalo nimelipeleka Kamati Kuu na Kamati Kuu wenyewe wameribariki na kulikubali sasa nataka nililete kwenu jina la kijana wetu Balozi Dk.Emmanuel Nchimbi kuwa mgombea mwenza,”amesema Rais Samia na baada ya kumaliza tu kutaja jina la Dk.Nchimbi kuwa mgombea mwenza wake wajumbe wa mkutano huo walionesha furaha zao kwa kupiga makodi , nderemo na vifijo.

Related Posts