Instagram Yabadili Mwonekano wa Ukubwa wa Picha – Global Publishers



Kama wewe ni mfuatiliaji mzuri wa mitandao ya kijamii hususan Instagram, utakuwa umeshagundua kwamba kuna mabadiliko yanayoendelea kwenye App hiyo kuhusu mwonekano wa ukubwa wa picha.

Kama ulikuwa unashangaa ni nini kinachoendelea, basi chukua hii!

Instagram imebadilisha ukubwa wa picha unazopost kutoka kwenye zile za ukubwa wa aspect ratio ya 1:1 (1080 x 1080 pixels) ambazo zina mwonekano wa mraba mpaka ukubwa wa aspect ratio ya 4:5 (1080 x 1350 pixels) ambazo zina mwonekano wa mstatili (potrait).

Mwonekano huu unaweza kuonekana vizuri kwenye ‘grid layout’, mpangilio wa mwonekano wa picha na video katika akaunti yako hasa unapotumia simu.

Miongoni mwa ‘influencers’ wakubwa Instagram, @sarahrichardssocial ameeleza kuwa watu wasiwe na hofu kwa sababu maboresho hayo, yanalenga kurahisisha zaidi namna ya kupiga picha na kuzipost Instagram.

“Hakuna picha itakayoondolewa, ni mwonekano tu utabadilika kwa hiyo na sisi lazima tubadilike.

“Unapopiga picha kwa kutumia simu ya android au iPhone, kamera zake zinapiga picha za ‘potrait by default’ kwa hiyo hutakuwa na ulazima wa kurekebisha chochote.











Related Posts