Dkt Mpango Alia na Wanaofumbia Macho Vitendo Vya Ukatili Nchini.

Makamo wa Rais wa Tanzania  Dkt Philiph Mpango amesema bado jamii inafumbia macho vitendo vya ukatili hali inayosababisha kushindwa kutoa taarifa katika mamlaka zinazohusika na kuzuia vitendo hivyo .

Mpango ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Chama cha Majaji na mahakimu Tanzania(TAWJA)uliofanyika Jijini Arusha kwa lengo la kupanga mikakati ya namna ya kutoa elimu kwa jamii juu ya vitendo vya ukatili sambamba na utoaji wa haki kwa waathirika wa vitendo hivyo.

Amesema kuwa  wapo watoto,wanawake na wanaume wanaopitia vitendo vya ukatili wa kijinsia au kimwili lakini hawatoi taarifa kwenye vyombo vya sheria.

“Mila na desturi zimekuwa zikichangia kwa kiwango kikubwa katika kuwakandamiza waathirika wa ukatili huo na kuwavunja moyo kuwa na uthubutu wa kutoa taarifa”Alisema Mpango

Amebainisha kuwa pamoja na dhamira njema iliyokuwa nayo Serikali katika kuhakikisha usawa wa kijinsia unakuwepo bado wanawake ambao ni nusu ya idadi ya wananchi lakini hawapewi nafasi ya umiliki wa mali kutokana na kubaguliwa kutokana na jinsia yao.

Awali wakati wa kumkaribisha mgeni rasmi jaji mkuu wa mahakama ya Tanzania Profesa Ibrahim Juma amesema Chama hiki cha Majaji na Mahakimu Wanawake kinaipa Mahakama uoni katika masuala ya

kijinsia na kwamba TAWJA imeipa Mahakama sura ya Taasisi inayojal Haki ya Kijinsia, Usawa wa Kijinsia na Kupinga ukatili na uonevu wote wa kijinsia.

Amesema kuwa Kupitia sherehe za Jubilei ya miaka 25 ya TAWJA,  Kwa miaka hii 25, huduma zimesambaa na kufikia jamii, na kufikisha taswira chanya ya Mahakama kwa jamii, hususani katika masuala ya usawa wa kijinsia.

Hata hivyo hafla ya ufunguzi wa maadhimisho ya Jubilei ya miaka 25 ya TAWJA imebeba kauli mbiu isemayo”Jubilei ya miaka 25 ya TAWJA kusherehekea utofauti na mshikamano katika usawa wa kijinsia”ambapo washiriki kutoka maeneo mbalimbali wameshiriki half hiyo.

Related Posts