MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)- Bara Tundu Lissu amesema pamoja na kutofautiana na Mwenyekiti wa Chama hicho Freeman Mbowe kwa misimamo lakini hawajawahi kugombana.
Akitoa Salamu zake leo Januari 21, 2025 kabla ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa chama hicho, Lissu amesema wanaweza kuwa wametofautiana kimsimamo lakini hawajawahi kugombana.
Amesema uamuzi wowote utakaofanywa na wajumbe wa chama hicho ni sehemu ya ujenzi wa chama naye ni muumini wa ujenzi wa chama hicho . “vyovyote itakavyokuwa leo nitakuwa mmoja wa kujenga chama chetu.”
Leo wajumbe wa chama hicho watafanya uchaguzi wa kumchagua Mwenyekiti wa chama huku mchuano mkali ukiwa kati ya Lissu na Mbowe lakini naye Odero Charles Odero akiwa hayupo nyuma kwenye mpambano huo
Katika uchaguzi huo wajumbe hao pia watamchagua Makamu Mwenyekiti Bara ambapo kuna mchuano mkali kati ya John Heche mjumbe wa zamani wa Kamati Kuu na Ezakia Wenje