Kambi ya matibabu yawekwa Ruangwa, Amana na Jai washirikiana “wananchi zaidi ya 3000”

Amana Bank na taasisi ya JAI kwa kushirikiana na ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa imefanikiwa kuandaa kambi ya matibabu inayoendeshwa na Madaktari bingwa na bingwa na bobezi katika fani mbalimbali kwa ajili ya kina mama na Watoto wa Wilaya ya Ruangwa na vijiji vya karibu.

Akizungumza katika kambi hiyo Meneja wa Sharia na bidhaa wa Amana bank Ndugu Salum Othman ameushukuru uongozi wa benki hiyo kwa uamuzi wake wa kufikisha huduma hizo kwa wananchi wa maeneo ya pembezoni mwa miji ambao wana uhitaji mkubwa zaidi wa huduma hizo.

Kambi hiyo inaendeshwa kwa muda wa siku tatu kuanzia Mei 12 – Mei 14 na Madaktari bingwa kutoka hospitali mbalimbali nchini na inatarajia kutoa huduma kwa wananchi zaidi ya 3,000.

Related Posts